Wastaafu waandamana hadi NSSF kushinikiza walipwe mafao yao
Bethsheba Wambura, Dar es Salaam Zaidi ya wanachama 200 wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), wamekusanyika katika Ofisi ya Mkoa wa Kinondoni wakishinikiza kulipwa mafao yao. Wastaafu hao wamekusanyika leo kuanzia saa sita mchana katika ofisi hizo Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam, ambapo wako waliostaafu kuanzia mwaka jana kurudi nyuma ambapo pamoja na mambo mengune wamedai hawajui ni kwanini hawalipwi mafao yao wakati Rais John Magufuli ametangaza wapewe mafao yao kwa wakati. Akizungumza na Mtanzania Digital mmoja wa wastaafu hao, Khamis Khamis, amesema yeye amestaafu tangu Juni mwaka 2018 lakini kila anapoenda kudai mafao yake anapigwa tarehe hali inayomfanya anashindwa kulipia watoto ada za shule ama kufungua biashara. Amesema wamekusanyika ili kupatiwa stahiki zao huku wakishinikiza kitumike kikotoo cha zamani na sio kile cha asilimia 33.3 kwani mtu anakuwa anadai fedha nyingi ila anapewa kidogo sababu tu sheria hairuhusu wakati Rais Magufuli alisema kila anayestaaf...






























Comments