Mrema atoa siri na mpango wa kurudi CCM

Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party TLP na Mwenyekiti wa bodi ya Parole amesema kuwa hawezi kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli kwa kumfuata ndani ya chama chake bali atafanya hivyo akiwa upinzani.
Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party TLP, Agustino Mrema na Rais Magufuli
Mrema ametoa kauli hiyo wakati akizungumza katika mahojiano maalum na www.eatv.tv ambayo ilitaka kupata maoni yake juu ya hamahama ya waliokuwa wabunge wa vyama vya upinzani ambao walieleza sababu kuu ya kufanya hivyo kuwa ni kumuunga mkono Rais Magufuli.
Mrema amesema, "sina sababu ya kurejea CCM, na ningetaka kurudi CCM hakuna wa kunizuia, ila narudi kufanya nini kwa sababu Rais aliniona nikiwa TLP, nirejee CCM kutafuta nini kama kazi nimepata na nawatumikia watanzania."
"Kuhusu kumuunga mkono Rais mimi nilimuunga mkono akiwa hajachaguliwa licha ya wenzangu wa upinzani walikuwa wamenitenga, kwa hiyo sirudi CCM kwa sababu Rais wangu hajaniambia nirudi CCM," ameongeza.
"Siamini kumfuata Rais CCM ndiyo kumuunga mkono, mbona mimi niko TLP na namuunga mkono, nampenda nitaendelea kuwaambia watanzania wamchague," amesema Mrema.
Mrema alishawahi kuwa Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi akiwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi ambaye alijibebea umaarufu kwa utendaji kazi wake lakini pia alishawahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Vunjo ambapo mwaka 2015 kiongozi huyo alienguliwa na Mbunge wa sasa James Mbatia.

Comments

Popular posts from this blog

KESI YA ZITTO MUSWADA WA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA YAHAMISHWA

Waziri asimamisha likizo za Marubani ATCL