Alichokisema Rais Magufuli mradi wa kuzalisha umeme

Mkataba huo umesainiwa leo Jumatano Desemba 12, Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo baada ya kusaini mkataba huo uliokuwa kati ya Rais John Magufuli na Waziri Mkuu wa Misri, Mostafa Madbouly, Watanzanaia wameombwa kuonesha ushirikiano wao kwa kuwa na mshikamano hadi hapo mradi huo utakapokamilika.
“Niwaombe wananchi wanaoishi kwenye vyanzo vya maji muunge mkono mradii huu kwa kutunza vyanzo vya maji, msichome miti hovyo na kwa bahati nzuri Wakuu wa Mikoa wote mko hapa,” amesema Magufuli.
Aidha, Rais Magufuli amesema mradi huo wa umeme wa Bonde la Mto Rufiji ulianza tangu kipindi cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, lakini kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo za kifedha nchi ilishindwa kutekelezajambo hilo.
Comments