Hakuna upungufu wa dawa" - Bohari ya Dawa


Mfumo wa ununuzi wa dawa wa pamoja kati ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na Taasisi ya Huduma za Afya ya Aga Khan umeelezwa kwamba utasaidia kupunguza gharama za dawa nchini Tanzania.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji, Lauren Bwanakunu wakati wa kusaini makubaliano ya ubia kati ya taasisi hizo mbili.
Amesema kwa kuagiza dawa kwa pamoja itasaidia kupunguza bei na kuwapunguzia mzigo wa gharama Watanzania.
Aidha ameongeza kwamba "Mkataba huu utawezesha kuendeleza na kugundua masoko na kuboresha shina la ugavi wa rasilimali pamoja na kuwatambua wauzaji wakuu ".
Pamoja na hayo Bwanakunu amesema mpaka sasa hakuna upungufu wa dawa ikiwemo dawa za magonjwa yasiyo ya kuambukiza pamoja na zile za magonjwa ya milipuko ikiwemo kipindupindu.

Comments

Popular posts from this blog

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja