Mbunge wa 10 kujiuzulu, arejea bungeni Skip to main content

Mbunge wa 10 kujiuzulu, arejea bungeni


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemtangaza Mgombea wa Ubunge jimbo la Temeke kupitia tiketi ya CCM, Abdallah Mtolea  kuwa Mbunge wa jimbo hilo baada ya kupita bila kupingwa.
Abdallah Mtolea, Mbunge mteule wa jimbo la Temeke.
Akitangaza ushindi huo Msimamizi wa Uchaguzi wilaya ya Temeke, Lusubilo Mwakabibi, amesema Mtolea ameshinda kiti hicho cha Ubunge baada ya wagombea wengine kushindwa kutimiza vigezo vya kugombea ikiwemo kukosea kujaza fomu.
"Abdallah Mtolea mgombea wa CCM, ameteuliwa kwakuwa ametimiza masharti yote kama kanuni zinavyoelekeza, na kwa mamlaka niliyopewa kwa mujibu wa sheria namtangaza ndugu Mtolea kuwa Mbunge mteule wa jimbo la Temeke", amesema Mwakabibi.
Mtolea alitangaza kujiuzulu nafasi yake hiyo na kisha kukihama chama chake cha CUF na kujiunga na CCM, ambapo Chama cha Mapinduzi (CCM), kilimpa nafasi ya kugombea Ubunge kwenye jimbo hilo kwa mara nyingine.

Comments

Popular posts from this blog

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja