zitambue hizi dalili 5 za Tezi Dume


Ugonjwa wa tezi tume imeelezwa ya kwamba ni miongoni mwa magonjwa ambayo yanasumbua jamii yetu kwa kiwango kikubwa sana na hata kupelekea kusababisha vifo.

Hata hivyo tafiti mbalimbali zinazidi kuonesha ya kwamba  wanaume ambao wanatumia pombe kali kwa kiwango kikubwa wapo hatarini kupata ugonjwa huo. Licha ya wanywaji wa pombe kali lakini inasadikika ya kwamba wanaume ambao wanafanya kazi za viwandani, husasani viwanda vya rangi au wanaofanya kazi ya kupaka rangi wapo hatarini kupata  ugonjwa huo.

Lakini pia wanaume ambao wapo hatarini kupata ugonjwa huo ni pamoja na wanaume wenye historia ya tatizo hili wenye familia zao, yaani wale ambao mmoja wa ndugu zake (kaka au mdogo wa kiume) au baba kama amewahi ugua ugonjwa huu.

Lakini pia watalamu mbalimbali wa masuala ya afya, wanazidi kueleza ya kwamba wanaume wenye umri wa kati ya miaka 40-70 wapo hatarini kupata ugonjwa huu wa tezi dumi.

Lakini licha ya kuendelea kusambaa kwa kasi kwa ugonjwa huu watalamu wa afya wanaeleza ya kwamba endapo ugonjwa huu wa tezi tume utaweza kutambulika mapema unaweza kutibika.

Dalili za ugonjwa  wa saratani dume.
Katika hatua zake za awali, dalili za saratani ya tezi dum hazitofautiani na zile za kuvimba kwa tezi dume (BPH). Dalili hizo ni pamoja na

1.    Kukojoa mkojo uliochnanganyika na damu.

2.    Kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku.

3.    Kukojoa mkojo wenye mtiririko mchafu.

4.    Kutirirka kwa mkojo baada ya kumaliza kukojoa.

5.    Kupata maamuvu wakati unapoanza kukojoa.

Comments

Popular posts from this blog

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja