Posts

Tundu Lissu anyoosha maelezo kuhusu kugombea Urais 2020

Image
Mwanasiasa wa upinzani nchini, Tundu Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki amesisitiza kuwa iwapo chama chake kitamteua kuwa mgombe wa urasi 2020 yupo tayari. Mwanasheria huyo Mkuu wa CHADEMA akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya BBC amesema yeye kugombea au kutogombea inategemea na maamuzi kutoka kwenye vikao vya chama chake. "Nimesema na ninaomba nirudie tena, kama chama changu na vyama tunavyoshirikiana navyo na Watanzania wanaotuunga mkono watasema kwamba mimi ninafaa, nipo tayari kufanya hivyo," amesema Tundu Lissu. Kwa sasa Tundu Lissu yupo katika ziara nchini Uingereza, moja ya lengo la ziara yake hiyo ni kueleza tukio la kushambuliwa na kujeruhiwa vibaya kwa risasi Septemba 17, 2017.

je, aacha mtoto mwema? Baba Mzazi wa Alikiba afariki Dunia

Image
Baba wa msanii wa msanii wa Bongo Fleva, AliKiba amefariki dunia. Mzee Saleh Kiba mefariki Dunia alfajiri ya leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa. Alikiba anafikwa na msiba wakati akiwa kwenye mchakato wa kuhakikisha kinywaji chake cha Mo Faya kinaingia sokoni.

Kangi Lugola afanya haya

Image
RAMADHAN HASSAN-DODOMA WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ametengua uteuzi wa makanda watatu wa polisi kutokana na kushindwa kutii maagizo yake pamoja na rushwa. Waliotenguliwa kuwa makamanda wa polisi wa mikoa ni makamanda wa polisi wa mikoa ya polisi ya Ilala (Salum Hamduni) na Temeke (Emmanuel Lukula) na Kamanda wa Mkoa wa Arusha, Ramadhan Ng’azi. Akizungumza na waandishi wa habari  Dodoma jana, Waziri Lugola alisema kabla ya kuchukua uamuzi huo, juzi alikutana na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama  ambao waliwapa maelekezo ya nini wanatakiwa kufanya kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri. Alisema   suala la makamanda wa polisi ambao wamesimamishwa imetokana na kushindwa kusimamia suala la rushwa jambo ambalo wameshindwa kulifanyia kazi eti kwa sababu yeye (aliyetoa agizo) ni mwanasiasa. “Kuna maelekezo nilitoa lakini kuna mikoa inabeza maelekezo hayo na maagizo hayafanyiwi kazi na mrejesho ninaopata ni kwamba maelekezo haya  hayafanyiwi kazi kw

Wapinzani: Spika tengua kauli yako

Image
SARAH MOSES -DODOMA KAMBI ya Upinzani Bungeni, imemtaka Spika wa Bunge, Job Ndugai, kutengua uamuzi wake wa kusimamisha vikao vya kamati za Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa ( LAAC ). Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dodoma jana, Mwakilishi wa Kambi ya Upinzani, John Mnyika alisema kauli aliyoitoa spika siyo ya Bunge, bali ni yake binafsi. “Haiwezekani mgogoro wa Spika na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Musa Assad, ukasimamisha mambo mengine ya  bunge kuendelea. “Kama kamati tunamtaka spika abadilishe uamuzi wake kwa kamati hizi mbili na awezeshe kamati hizo kukutana kabla ya tarehe 25 mwezi huu,”alisema Mnyika na kuongeza: “Tumesikia spika amesimamisha kamati hizo kwa kuwa CAG ameitwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Januari 21, mwaka huu  kwa kile alichokiita mgogoro wa  CAG na Bunge … kauli hiyo siyo ya Bunge ila ni yake binafsi”. Alisema uamuzi alioutangaza Spika

Katibu baraza la ardhi kortini

Image
BENJAMIN MASESE MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Geita imehukumiwa Katibu wa Baraza la Kata la Nyamboge, Theleza Barnabas, kifungo cha miaka mitano au kulipa sh 200,000  kila kosa  kwa kupatikana na  hatia  ya kuomba na kupokea rushwa. Alilipa faini na kuachiwa.  Akitoa hukumu,  Hakimu  wa mahakama hiyo, Jovith Kato alisema  mahakama ilizingatia ushahidi wa jamuhuri na ushahidi wa utetezi.  Awali,  Mwendesha Mashitaka wa Takukuru, Dennis Lekayo alidai   Septemba  13, 2018 katika Kata ya Nyamboge  wilayani Geita, mshitakiwa aliomba rushwa ya Sh 200,000 kutoka kwa Sanda Magohe   amsaidie kupata ushindi kwenye shauri la ardhi namba 01/2018 dhidi ya Dotto Maonyole lilokuwa linasikilizwa na Baraza la Kata ya Nyamboge. Baada ya kuombwa rushwa hiyo,   Sanda ambaye alikuwa ni mlalamikaji katika shauri hilo, aliamua kutoa taarifa hiyo kwa Takukuru Mkoa wa Geita ambako mtego uliandaliwa kwa kutumia fedha za mtego. Alisema Septemba 20, 2018 Sanda alimpelekea fedha h

SOMA HIYO!:Wananchi wahamasishwa kubangua korosho

Image
HADIJA OMARY-LINDI MKUU wa Wilaya ya Lindi, Shahibu Ndemanga, amewataka wajasiriamali wilayani hapa kuchangamkia fursa ya ubanguaji wa korosho iliyotolewa na Serikali ili waweze kujikwamua kiuchumi. Ndemanga aliyasema hayo mjini hapa jana alipokuwa akifunga mafunzo ya ubanguaji bora wa korosho yaliyotolewa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo Vidogo (Sido), Mkoa wa Lindi. Ndemanga alisema kwamba, Serikali ilipoamua korosho zote zibanguliwe ndani ya nchi, ilikuwa na lengo la kuinua uchumi wa wananchi wake na kwamba wananchi wanatakiwa kutumia fursa hiyo ili kuinua uchumi wao. “Uamuzi wa Sido wa kuwakusanya wajasiriamali na kuwapa mafunzo ya ubanguaji bora wa korosho ni kitendo cha kizalendo kwani kitawafanya wajasiriamali kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya ubanguaji  vitakavyowaongezea kipato,” alisema Ndemanga. Naye Ofisa Uendelezaji Mafunzo kutoka Sido, Aizack Daniely, alisema  katika mafunzo hayo ya siku tano yenye lengo la kuongeza kasi ya uongezaji wa thamani katika zao la

Kidato cha kwanza waruhusiwa kuvaa sare za shule ya msingi

Image
  Kidato cha kwanza waruhusiwa kuvaa sare za shule ya msingi Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri ametoa ruhusa kuvaa sare za elimu ya msingi kwa wanafunzi ambao wamefanikiwa kufaulu elimu ya msingi na kushindwa kujiunga na elimu ya Sekondari kutokana na wazazi kushindwa kukamilisha mahitaji hayo. Ametoa ruhusa hiyo alipotembelea katika shule ya Sekondari Maheve iliyopo katika Kata ya Ramadhani pamoja na shule ya Sekondari Joseph Mbeyela zilizopo halmashauri ya mji wa Njombe na kupata taarifa ya baadhi ya wanafunzi kushindwa kufika shuleni kutokana na kukosa baadhi ya mahitaji kama sare za shule. “Hawa wanafunzi si walikuwa wanasoma, sasa hawa watoto waje na uniform zao za shule za msingi waje na chakula wakati wazazi wanaendelea kukamilisha

INATISHA! Akutwa Amekufa Kwenye Kiroba Dar – VIDEO

Image
MWILI wa mtu mmoja ambaye jina lake halijajulikana umekutwa ukiwa umefungwa kwenye kiroba na kutupwa kando ya barabara katika eneo la Karibu na Chuo cha Ustawi wa Jamii mkabala na Ofisi za Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kilichopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Mtu huyo ambaye hakufahamika hata jinsia yake kutokana na namna ambavyo kiroba hicho kilikuwa kimefungwa juu na chini, anadaiwa huenda aliawa na mwili wake kutupwa ndani ya mfereji katika eneo hilo. Global TV Online imefunga safari mpaka eneo la tukio na hii ndiyo hali halisi ilivyokuwa baada ya kuukuta mwili huo huku wananchi wa eneo hilo wakihamaki kutokana na tukio hilo la kinyama.

HABARI ZA LEO ALHAMISI Januari 17, 2019

Image
Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo ALHAMISI january 17, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.

Abdul Nondo aja kivingine, ‘Huu muswada haufai

Image
Mwanaharakati kijana, Abdul Nondo amesema kuwa baadhi ya vifungu vilivyomo kwenye muswada wa sheria ya vyama vya siasa, vinahitaji kufanyiwa marekebisho ili kuendana na uhalisia wa demokrasia nchini. Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media mara baada ya kumalizika kwa Kongamano la kutoa maoni kuhusu muswada huo lililoandaliwa na chama cha mapinduzi (CCM), ambapo amesema vifungu hivyo vinatakiwa kutolewa ili muswada huo uweze kuimarisha demokrasia nchini. ”Muswada huu unahitaji kufanyiwa marekebisho makubwa, kuna vifungu ndani yake vinatakiwa kuondolewa kabisa ili tuweze kukuza uhai wa demokrasia yetu hapa nchini,”amesema Nondo

Spika: Tumesitisha kufanya kazi na CAG

Image
MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM SPIKA wa Bunge Job Ndugai, amesema kwa sasa Bunge limesitisha kufanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad. Kutokana na hali hiyo, amewatawanya wajumbe wa Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na ile ya Hesabu za Serikali za Tawala za Mikoa na Mitaa (LAAC) kufanya kazi katika kamati nyingine. Hatua ya usitishaji huo inatokana na kauli ya Profesa Assad aliyoitoa Desemba mwaka jana katika mahojiano na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, Arnold Kayanda. Mtangazaji huyo alimuuliza CAG kuwa ni vipi ofisi yake imekuwa ikijitahidi kila mwaka kufanya ukaguzi na kutoa ripoti zenye kuonesha kuna ubadhirifu, lakini baada ya hapo wananchi hawaoni kinachoendelea. Katika majibu yake CAG alisema; “Hilo ni jambo ambalo kimsingi ni kazi ya Bunge. Kama tunatoa ripoti zinazoonyesha kuna ubadhirifu halafu hatua hazichukuliwi, huo kwangu ni udhaifu wa Bunge. “Bunge linatakiwa kus

Kangi Lugola amtaka Musilimu kujipima, atumbua makamanda watatu

Image
Ramadhan Hassan, Dodoma Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amemtaka Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Musilimu, kujitafakari kutokana na rushwa iliyokithiri na uonevu kwa wenye magari. Kauli hiyo ameitoa leo Jumatano Januari 16, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ambapo amedai kwamba kumekuwa na utaratibu wa askari wa usalama barabarani kuwabambikizia watu kesi huku wakichukua rushwa wazi wazi bila kificho. “Askari wa barabarani wamekuwa wakiwatoza watu kwa makosa ambayo hayaeleweki, namuomba Kamanda wa Usalama Barabarani ajitafakari,” amesema. Katika hatua nyingine Waziri huyo wa Mambo ya Ndani ya Nchi amewasimamisha kazi makamanda watatu wa polisi kwa makosa mbalimbali ikiwemo kutotii maagizo yake. Makamanda waliosimamishwa kazi ni pamoja na wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala Salum Hamduni, Temeke, Emanuel Lukula na wa Arusha Ramadhan Ng’azi. “Sababu za kuwasimamisha Kamanda wa Ilala na Temeke

CCM yaifagilia Sheria Mabadiliko ya Vyama vya Siasa

Image
Elizabeth Joachim, Dar es Salaam Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, amesema sheria vya vyama vya siasa iliyopo sasa haimpi nguvu Msajili wa Vyama vya Siasa kufanya kazi kwa ufanisi hivyo mabadiliko ya muswada mpya yatasaidia uimara wa vyama vya siasa na Ofisi ya Msajili kufanya kazi kwa ufanisi. Polepole ameyasema hayo leo Jumatano Januari 16 katika mkutano wa chama hicho wa kujadili mabadiliko ya muswada kabla ya kupelekwa Bungeni uliofanyika Jijini Dar es Salaam. “Mabadiliko hayo yatampa nguvu msajili wa vyama vya siasa kutazama kwa jicho la upole endapo chama kimefanya vizuri na jicho la ukali kwa mambo ya ovyo ambayo hama kitafanya,” amesema. Aidha, amesema mabadiliko hayo yatampa nguvu Msajili kuhusika kwenye usajili wa vyama vya siasa, kusimamia chaguzi za vyama vya ndani, kutoa na kufuatilia uwajibikaji wa ruzuku. “Sheria tunayoitumia sasa ni sheria ya mwaka 2010 ni miaka 10 imepita tangu kufanya mabadiliko ya s

SOMA HIYOO! Magaidi walioshambulia hoteli Nairobi wafanyiwa hivi

Image
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema kuwa magaidi waliohusika kufanya shambulio la kuvamia hoteli la kifahari ya DusitD2 iliyopo nchini Kenya jijini Nairobi tayari wameuawa na operesheni imekamilika. Hata hivyo shambulio hilo limeleta madhara makubwa ikiwemo kusababisha vifo vya watu 14 pamoja na majeruhi huku wengine 700 wakiwa wamefanikiwa kuokolewa katika janga hilo lililoikumba nchi ya Kenya siku ya jana. Ambapo kundi la kigaidi la Al-shabaab limekiri kuhusika na shambulio hilo ambapo jana majira ya saa 9 jioni walivamia hoteli hiyo na kufanya shambulio hilo katika eneo la 14 Riverside. Shambulio hilo la kigaidi lililotajwa kufanywa na watu sita lililohusisha milio ya risasi pamoja na mabomu yaliyotawala na kusababisha vurugu kubwa katika eneo hilo. Aidha hali ya sasa ni shwari mara baada ya jeshi la polisi pamoja na vyombo vingine vya usalama kumaliza operesheni hiyo ya kufanya jiji litulie na kuwa na amani baada ya mtikisiko huo.

LIVE: Rais Magufuli akipokea hati za utambulisho wa Mabalozi

Image
Fuatilia hapa moja kwa moja kutoka Ikulu jijini Dar es salaam, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akipokea hati za utambulisho wa mabalozi mbalimbali leo Januari 16, 2019

HABARI ZA LEO JUMATANO 16/1/2019

Image