Kidato cha kwanza waruhusiwa kuvaa sare za shule ya msingi



  Kidato cha kwanza waruhusiwa kuvaa sare za shule ya msingi
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri ametoa ruhusa kuvaa sare za elimu ya msingi kwa wanafunzi ambao wamefanikiwa kufaulu elimu ya msingi na kushindwa kujiunga na elimu ya Sekondari kutokana na wazazi kushindwa kukamilisha mahitaji hayo.
Ametoa ruhusa hiyo alipotembelea katika shule ya Sekondari Maheve iliyopo katika Kata ya Ramadhani pamoja na shule ya Sekondari Joseph Mbeyela zilizopo halmashauri ya mji wa Njombe na kupata taarifa ya baadhi ya wanafunzi kushindwa kufika shuleni kutokana na kukosa baadhi ya mahitaji kama sare za shule.
“Hawa wanafunzi si walikuwa wanasoma, sasa hawa watoto waje na uniform zao za shule za msingi waje na chakula wakati wazazi wanaendelea kukamilisha hayo na mahitaji mengine, hawa wanafunzi kama na tatizo hilo waendelee kusoma kwasababu tayari wanacheleweshwa masomo,”amesema Msafiri
Aidha ameongeza kuwa kwa wanafunzi ambao wameshindwa kupata daftari za kuandikia ni vyema wakafika shuleni na Madaftari yao ya shule ya msingi waliyokuwa wakiyatumia kwa kuwa walikuwa wanasoma wakati wazazi wakiendelea kukamilisha mahitaji hayo.
Hata hivyo, Halmashauri ya Mji wa Njombe Ilifanikiwa kufaulisha Jumla ya Wanafunzi 3001 ambapo Kati Yao 572 Walielezwa Kukosa nafasi Kutokana na Uhaba wa Madarasa Jambo lililowalazimu Kuwapeleka Kwenye kata nyingine ambazo hazina upungufu wa madarasa wakati baadhi ya wanafunzi wakionekana kutokufika shuleni kutokana na changamoto mbalimbali katika familia zao.
ACADEMIC BOOKS
EXAMINATION RESULTS

Comments

Popular posts from this blog

KESI YA ZITTO MUSWADA WA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA YAHAMISHWA

Waziri asimamisha likizo za Marubani ATCL