Atolewa Hospitali Nchini Ujerumani
Staa wa Bongo Fleva, Omary Nyembo. MUNGU mkubwa! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya staa wa Bongo Fleva, Omary Nyembo kutolewa katika hospitali ya University Hospital of Dusseldorf ya nchini Ujerumani alikokuwa amelazwa baada ya kupata nafuu na kupelekwa Mombasa nchini Kenya. Akizungumza na Risasi Jumamosi, baba mzazi wa staa huyo, Faraji Nyembo alisema anamshukuru Mungu na Watanzania kwa maombi yao kwani mwanaye huyo kwa sasa ana nafuu na amepelekwa Kenya kwa ajili ya kuhudhuria kliniki. Aliendelea kueleza kuwa kwa sasa afya ya Dimpoz imeendelea kuimarika ambapo amefanikiwa kuruhusiwa kutoka hospitali ikiwa ni baada ya kufanyiwa oparesheni kubwa ya koo na sasa yupo nchini Kenya anakofanya kliniki pamoja na kupumzika pia. “Mwanangu sasa anaendelea vizuri kwani upasuaji aliofanyiwa umempa nafuu na hivi ninavyoongea na wewe ameruhusiwa kutoka hospitali nchini Ujerumani na yupo Kenya anakofanyia kliniki yake akisimamiwa na meya wa Mombasa ambaye ndiye anayempatia m...




































Comments