Abdul Nondo aja kivingine, ‘Huu muswada haufai
Mwanaharakati kijana, Abdul Nondo amesema kuwa baadhi ya vifungu vilivyomo kwenye muswada wa sheria ya vyama vya siasa, vinahitaji kufanyiwa marekebisho ili kuendana na uhalisia wa demokrasia nchini.
Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media mara baada ya kumalizika kwa Kongamano la kutoa maoni kuhusu muswada huo lililoandaliwa na chama cha mapinduzi (CCM), ambapo amesema vifungu hivyo vinatakiwa kutolewa ili muswada huo uweze kuimarisha demokrasia nchini.
”Muswada huu unahitaji kufanyiwa marekebisho makubwa, kuna vifungu ndani yake vinatakiwa kuondolewa kabisa ili tuweze kukuza uhai wa demokrasia yetu hapa nchini,”amesema Nondo
Comments