CCM yaifagilia Sheria Mabadiliko ya Vyama vya Siasa


Elizabeth Joachim, Dar es Salaam
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, amesema sheria vya vyama vya siasa iliyopo sasa haimpi nguvu Msajili wa Vyama vya Siasa kufanya kazi kwa ufanisi hivyo mabadiliko ya muswada mpya yatasaidia uimara wa vyama vya siasa na Ofisi ya Msajili kufanya kazi kwa ufanisi.
Polepole ameyasema hayo leo Jumatano Januari 16 katika mkutano wa chama hicho wa kujadili mabadiliko ya muswada kabla ya kupelekwa Bungeni uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
“Mabadiliko hayo yatampa nguvu msajili wa vyama vya siasa kutazama kwa jicho la upole endapo chama kimefanya vizuri na jicho la ukali kwa mambo ya ovyo ambayo hama kitafanya,” amesema.
Aidha, amesema mabadiliko hayo yatampa nguvu Msajili kuhusika kwenye usajili wa vyama vya siasa, kusimamia chaguzi za vyama vya ndani, kutoa na kufuatilia uwajibikaji wa ruzuku.
“Sheria tunayoitumia sasa ni sheria ya mwaka 2010 ni miaka 10 imepita tangu kufanya mabadiliko ya sheria, sisi ni vijana tunatakiwa tutoe maoni na mabadiliko ya sheria mpya ili sheria mpya itakayokuja kutumika isiweze kumbana msajili wa vyama vya siasa pamoja na sisi wanachama,” amesema Polepole.

Comments

Popular posts from this blog

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja