INATISHA! Akutwa Amekufa Kwenye Kiroba Dar – VIDEO
MWILI wa mtu mmoja ambaye jina lake halijajulikana umekutwa ukiwa umefungwa kwenye kiroba na kutupwa kando ya barabara katika eneo la Karibu na Chuo cha Ustawi wa Jamii mkabala na Ofisi za Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kilichopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Global TV Online imefunga safari
mpaka eneo la tukio na hii ndiyo hali halisi ilivyokuwa baada ya kuukuta
mwili huo huku wananchi wa eneo hilo wakihamaki kutokana na tukio hilo
la kinyama.
Comments