KESI YA ZITTO MUSWADA WA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA YAHAMISHWA

Shauri la kesi hiyo lilipangwa kusikilizwa na Majaji; Barke Sehel (kiongozi wa jopo), Benhajo Masoud na Salma Maghimbi, lakini limekwama baada ya wajibu maombi (Serikali) kuwasilisha pingamizi la awali wakiitaka Mahakama hiyo ilitupilie mbali.
Aidha, kutokana na pingamizi hilo, Mahakama imesitisha usikilizwaji wa shauri la msingi na badala yake imeamua kuanza kusikiliza pingamizi ambapo imepanga kusikiliza pingamizi hilo na jaji Masoud katika chemba kuanzia saa 4:00, asubuhi.
Comments