Posts

Tabora:Wauguzi wanaotoa lugha chafu waonywa

Image
WAUGUZI na watoa huduma za afya wa zahanati, vituo vya afya na hospitali mkoani Tabora, wametakiwa kufuata maadili ya kazi yao na kuacha kutoa lugha chafu zenye maudhi au kebehi kwa akinamama wajawazito wanaoenda kupata huduma. Onyo hiyo, limetolewa juzi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Tabora, Mwajuma Mhina ambaye alisema baadhi ya akinamama wakiwemo wajawazito wamekuwa wakitendewa ukatili na wauguzi kwa kutolewa lugha chafu afya jambo ambalo ni kinyume na maadili ya kazi hiyo. Alisema wauguzi kama hao hawawezi kufumbiwa macho kwa kuwa vitendo vya vinadhalilisha utu wa mwanamke na kuwaomba kutoa huduma kwa kuzingatia maadili na misingi ya kazi. “Huu ni unyanyasaji kwa akinamama, unawezaje kutoa lugha zisizofaa wakati wa mgonjwa akihitaji umuhudumie, umesomea kuwahudumia huo ndiyo wajibu wako utimize.., lakini kwa kuwa wapo wasiosikia tunaiomba Serikali kupitia wizara ya afya kufuatilia na kuwachukuliwa hatua,”alisema. Al

Z’bar: Naibu waziri atoa mazito kwa wanafunzi

Image
Na Khamis Sharif-ZANAIBAR NAIBU Waziri wa  Wizara  ya Kazi, Uwezeshaji,  Wazee ,Wanawake na Watoto, Shadya Mohamed Suleiman amewataka wanafunzi wa Jimbo la Magomeni kushughulikia masomo yao na kujiepusha na mambo ya tamaa kwani  yanaweza kuwapelekea kutofikia malengo yao. Hayo aliyasema hivi karibuni alipokuwa akizungumza katika utaoji wa zawadi katika shule za Jimbo la Magomeni wakati wa sherehe ya utoaji wa zawadi kwa wanafunzi waliofaulu kuingia michepuo , kidato cha pili na kidato cha tano kwa mwaka 2017/2018. Alisema ili wafanikiwe zaidi katika elimu ni lazima wawe wasikivu na wavumilivu kwa kufuata ushauri wa walimu ndipo watafanikiwa kwani elimu ndio mustakabali mzima wa maisha  na kuwataka waongeze bidii katika masomo  kwani wao ndio wataalamu  watarajiwa wa hapo baadae. “Acheni tamaa za kutamani vitu ambavyo wazazi hawana uwezo navyo mambo haya ndio yanayoweza kukuharibieni malengo yenu mliojiwekea ya baadae shuhulikieni masomo yenu,” a

CCM Morogoro watoa sifa hizi

Image
i Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Morogoro kimewataka wananchi wote kumpa moyo Rais Dk. John Magufuli, kwani kazi anayoifanya chini ya serikali yake ni ya kishujaa kwa Watanzania wote. Pamoja na hali hiyo chama hicho kimewataka wananchi kuzidisha bidii ya kazi na uzalishaji wenye tija kwa manufaa pindi wanapokuwa kwenye ofisi zao, viwandani au mashambani. Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Innocent Kalogeresi alisema wananchi, viongozi , wanaharakati  na wanasiasa , wote  wana wajibu wa kutokuwa wepesi kurubuniwa au kununuliwa utu wao kwa kushiriki  usaliti. “Rais Magufuli ni shujaa wa kweli wa maendeleo katika Taifa letu na kwa hali hii Watanzania wote kwa umoja na mshikamano wetu tumpe ushirikiano wa kila aina. “Tanzania ni moja na itabaki moja daima kwani  ni miongoni mwa nchi yenye hazina kubwa katika nchi za Kusini mwa Afrika iliohifadhi wapigania uhuru,” alisema Ka

Kampuni ya Setewico yalia

Image
Na MWANDISHI WETU-DODOMA UTITIRI wa kodi ambazo zinalipwa na wawekezaji nchini bado umeonekana kuwa changamoto kubwa kwao na hivyo kutoa ombi kwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk. John Magufuli kuangalia namna ya kupunguza utitiri huo wa kodi hizo. Ombi hilo limetolewa hivi karibuni jijini hapa na Mkurugenzi wa Ushirikiano na Uhusiano wa Jamii wa Kampuni ya Cetewico Limited,  Katrin Boehl alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliofanya ziara katika kiwanda hicho. “Kwa upande wangu lazima niseme nimeona ushirikiano wa hali ya juu  katika Serikali yangu Dodoma kwani nikiwa na tatizo lolote ninakwenda katika ofisi za Serikali yangu ya Dodoma, hivyo imeonesha uthamini  wa kiwango kikubwa wa  kazi tunazofanya,” alisema Katrin. Alisema kampuni yao inapongeza juhudi za Serikali katika ujenzi wa Tanzania ya viwanda nchini ili kufikia uchumi wa kati na wamedhamiria kuunga mkono kwa vitendo kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu lakini changamoto kubwa amb

BoT yataja faida za dhamana za serikal

Image
Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM WATANZANIA wameshauriwa kushiriki kikamilifu katika minada ya dhamana za Serikali kwani faida zake ni kubwa kwa Taifa ikiwamo kufanya shughuli za maendeleo kwa kutumia fedha zake za ndani. Hayo yamesemwa hivi karibuni mjini Dodoma na Mkurugenzi wa Masoko na Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT),  Alexander Ng’winamila wakati akiwasilisha mada katika mafunzo kwa waandishi wa habari za uchumi na fedha yalioandaliwa na BoT kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuandika habari za fedha na uchumi. Akizungumza wakati akitoa mada inayohusu uwekezaji katika dhamana za Serikali; faida zake kwa Taifa na wawekezaji ambapo pamoja na mambo mengine amezungumzia umuhimu wa wananchi kushiriki kikamilifu kwenye midana ya dhamana za Serikali. Alisema bado kuna haja kwa vyombo vya habari kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kujua na kushiriki kikamilifu  katika minada hiyo. “Ombi letu kwa vyombo vya habari tunaomba muendelee kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa

jifunze kufaham ugonjwa Wa Chango La Uzazi - (Mke/Mume)

Image
Tunapozungumzia mgonjwa wa chango tuna maana kuwa ni matatizo yaliyopo katika viungo vya uzazi kwa mke au mume. Huu ni ugonjwa ambao humpata mtu katika umri mdogo utotoni. Kwa mfano :- mume, hupata maumivu ya tumbo mara kueneza anapokuwa mdogo. Kwa upande wa mwanamke hupata maumivu ya tumbo anapoanza kuvunja ungo. Maumivu hayo hupelekea mtu (mume/mwanamke) kupata madhara katika viungo vyake vya uzazi. DALILI ZAKE Kwa mwanaume atakuwa akishiriki tendo la ndoa, anawahi sana kufika kileleni na kurudia mara nyingine ni vigumu sana. Pia mwanaume hatakuwa na uwezo wa kusimamisha. Ni vigumu kumpa mimba mwanamke Mwanamke mwenye chango la uzazi ana dalili zifuatazo:- Kupata maumivu makali wakati anapokaribia kuingia katika siku zake za hedhi Kuhisi maumivu makali wakati wa kushiriki tendo la ndoa Siku zake za hedhi hazitakuwa na ratiba, zitakuwa zinabadilika badilika Hujisikia homa kali anapokaribia siku zake za dhedhi Kupatwa hasirakali/ jazba anapokaribia kuingia kat

Askari polisi amchoma mwanafunzi kwa pasi ya umeme

Image
Tukio hili limetokea  tarehe 20/12/2018 majira ya 19:30hrs ambapo Jeshi la Polisi lilipata taarifa kuwa huko maeneo ya Mtaa wa Lumaliza kata ya Mbugani Manispaa ya Tabora  kijana mmoja aitwaye  JUMANNE NTIMIZI, HUSSEIN, Miaka 17, Mwanafunzi kidato cha tatu katika shule ya sekondari Cheyo, alijeruhiwa na Askari  anayefahamika kwa jina la E.9301 CPL ALMAS   kwa kuchomwa  na pasi ya umeme sehemu mbalimbali za mwili wake na kisha kupigwa na kitu kizito kwenye paji la uso, mdomoni na kumsababishia maumivu makali mwilini. Chanzo cha tukio hili ni kutokana na  kijana JUMANNE NTIMIZI kukutwa  na bwana ALMAS  akiwa amemkumbatia binti yake aitwaye AMINA ALMASI, Miaka 17, Mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Cheyo karibu na nyumba yake  kwa nia ya kufanya mapenzi ndipo baba mzazi wa Binti huyo alipochukua hatua ya kufanya kitendo hicho kibaya. Akiongea na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora    ACP – EMMANUEL NLEY amesema  Jeshi la Polisi mkoa wa

MAGAZETI YA LEO 26/12/2018

Image

Maajabu! :Mwanafunzi mdogo alawiti watoto wenzake,polisi wamtafuta

Image
Mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi ya Wilunze mwenye umri wa miaka 14 anatuhumiwa kuwalawiti wanafunzi wenzake ambapo katika tukio la hivi karibuni alimlawiti mtoto wa miaka mitatu. Hayo yalibainishwa na Mtendaji wa Kijiji Cha Wilunze Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Georgina Richard wakati akizungumza juzi katika mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa vijiji na kata kupitia mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia, mimba na ndoa za utotoni unaotekelezwa na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Woman Wake Up (WOWAP). Alieleza kuwa tukio la kulawitiwa mtoto wa kiume wa miaka mitatu lilitokea Novemba 26, mwaka huu kijijini hapo. Alisema mtuhumiwa huyo ni mtoro wa kudumu na mara ya mwisho alikuwa akisoma darasa la tatu Shule ya Msingi Wilunze. Alisema siku ya tukio mtuhumiwa huyo alimuingiza mtoto huyo kwenye nyumba ambayo haijamalizika na kumfanyia kitendo hicho. “Aliyeshuhudia kitendo hicho ndio alikwenda kutoa taarifa kwa mama wa mtoto ambapo

Mawakala 10 wa Shirika la Ndege Tanzania Kizimbani kuhujumu uchumi

Image
Mawakala 10 wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi ikiwamo kulisababishia Shirika hasara, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha Sh. milioni 10.8. Washtakiwa hao walisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ally Salum. Wakili wa Serikali, Wankyo Simon, aliwataja washtakiwa hao kuwa ni, Fabian Ishengoma (34), Adam Kamara (27), Marlon Masubo (29), Neema Kisunda (24), Alexander Malongo (29) na Tunu Kiluvia (32). Wengine ni Jobu Mkumbwa (30), Mohammed Issah (38), Godfrey Mgomela, Absalom Ambilikile na Janeth Lubega. Upande wa Jamhuri ulidai kuwa kati ya Machi 10 na Oktoba 9, mwaka huu, mahali tofauti jijini Dar es Salaam na Mwanza washtakiwa kwa pamoja wakiwa mawakala wa ATCL, walilisababishia Shirika hilo hasara ya Sh.10,874,280. Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa tarehe na mahali pa shtaka la kwanza, washtakiwa wote kwa pamoja walijipatia fedha

Takukuru mwanza yashinda kesi

Image
Na Paschal D.Lucas,Mwanza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza, imeshinda kesi Na. 15/2018 dhidi ya Maafisa Elimu wawili Bw. MUGUSI RICHARD ISANGA- Afisa Elimu Jiji la Mwanza na Bw. JAPHET MWIKABE BUCHA wa Manispaa ya Ilemela. Mnamo tarehe 06/02/2018 washitakiwa  walifikishwa Mahakamani kwa kosa  la kuomba na kupokea Rushwa ya sh 1,000,000/= kutoka kwa  Mwananchi  ili waweze kumsaidia mtoto wake kupata nafasi ya shule ya Bweni, ambapo ni kinyume na kifungu cha 15 (1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2007. Mnamo tarehe 14.12.2018, hukumu ya kesi hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mheshimiwa  RODA NDIMILANGA ambapo  washitakiwa walikutwa na hatia na Mahakama ikawaamuru adhabu ya faini ya shilingi laki tatu (Tsh. 300,000/=) au kifungo cha miaka mitatu (3) jela kwa kila mmoja.

Msaidizi wa waziri ashikiliwa kwa tuhuma za kubaka

Image
Kwa kipindi cha wiki moja Jumla  ya makosa matano ya udhalilishaji yameripotiwa katika vituo mbali mbali ndani ya mkoa wa mjini magharib unguja. Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo kwa waandishi wa Habari  Kamanda wa Jeshi La Polisi mkoa wa Mjini Unguja Thobias Sedoyeka alisema katika Matukio hayo watuhumiwa watatu wamekamatwa akiwemo Shabani Ali Othman miaka 32 Mkaazi wa Mpendae ambaye ni msaidizi binfsi wa waziri. Alisema Shaban anadaiwa kutenda kosa hilo Novemba 18 mwaka huu saa 10:00 jioni katika ofisi ya serikali, Maruhubi. Alisema mtuhumiwa anadaiwa kumpa kinywaji mshichana (jina linahifadhiwa) ambae pia ni mfanyakazi mwenzake na kusababisha kupoteza fahamu na hatimae kumbaka. Alisema uchunguzi bado unaendelea huku taratibu za kumfikisha mahakani mshitakiwa zikiendelea. Pia alisema jumla ya matukio matatu ya vifo yameripotiwa ambayo yalitokea baina ya Disemba 17 na 21 katika maeneo tofauti ya mkoa huo. Alisema Disemba 17 saa 10:00 jioni katika pwan

Bunge lavunjwa kuitisha uchaguzi mpya 2019

Image
Viongozi wa vyama vinavyounda Serikali ya Mseto ya Israel wamekubaliana kulivunja Bunge na kuitisha uchaguzi  mpya Aprili 2019. Baada ya mkutano wa leo Jumanne kwa sauti moja wamekubaliana kuvunja Bunge na kuitisha uchaguzi mapema baada ya muhula wa miaka minne. Hatua hiyo imefikiwa huku kukiwa na mvutano ndani ya Serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ya siasa za mlengo wa kulia. Netanyahu amekabiliwa na shinikizo la madai ya ufisadi, huku waendesha mashtaka wakimtafutia sababu za kumfungulia mashtaka tokea mwanzoni wa mwaka. Hata hivyo, ripoti zinasema kuwa Mkuu wa zamani wa Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF), Benny Gantz, anajiandaa kugombea kama mgombea binafsi hali ambayo inaweza kusababisha ugumu wa kutabiri matokeo. Netanyahu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Likuda amehudumu kama Waziri Mkuu wa Israel tangu 2009 mpaka sasa.

JITIBU JIPU KWA DAW HII

Image
Bilinganya ni kiungo ambacho hutumika kuongeza / kuleta ladha katika mboga. Pamoja kuwa ni kiuongo ambacho hutumika kuongeza ladha katika mboga pia Ikumbukwe ya kwamba bilinganya ni tunda ambalo ni dawa, ambapo hutumia kutibu magonjwa yafuatayo; Vidonda vya tumbo. Linasaidia sana kwa watu wenye matatizo ya kukosa usingizi wanashauri kula kwa wingi. Pia kwa wale wenye matatizo ya  homa, Ikumbukwe bilinganya husaidia mtu kuwa na afya nzuri ya mwili pindi atakapolitumia. Kwa wale wenye matatizo ya jipu kumbuka ya kwamba bilinginya ni dawa tosha juu ya tatizo hilo, unachotakiwa kufanya ni kwamba lipondeponde kisha uweke katika jibu. Pia kama utaamua kutengeneza jusi yake, inaaminika ya kwamba tunda hili lina uwezo madhubuti wa kuondoa sumu zote zilizopo mwilini. Endelea kutembelea Muungwana Blog kila wakati ili kupata masomo mengine mengi kama haya kila siku. Asante

HABARI ZA LEO 25/12/2018

Image