Takukuru mwanza yashinda kesi

Na Paschal D.Lucas,Mwanza
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza, imeshinda kesi Na. 15/2018 dhidi ya Maafisa Elimu wawili Bw. MUGUSI RICHARD ISANGA- Afisa Elimu Jiji la Mwanza na Bw. JAPHET MWIKABE BUCHA wa Manispaa ya Ilemela.

Mnamo tarehe 06/02/2018 washitakiwa  walifikishwa Mahakamani kwa kosa  la kuomba na kupokea Rushwa ya sh 1,000,000/= kutoka kwa  Mwananchi  ili waweze kumsaidia mtoto wake kupata nafasi ya shule ya Bweni, ambapo ni kinyume na kifungu cha 15 (1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2007.

Mnamo tarehe 14.12.2018, hukumu ya kesi hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mheshimiwa  RODA NDIMILANGA ambapo  washitakiwa walikutwa na hatia na Mahakama ikawaamuru adhabu ya faini ya shilingi laki tatu (Tsh. 300,000/=) au kifungo cha miaka mitatu (3) jela kwa kila mmoja.

Comments

Popular posts from this blog

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC