Askari polisi amchoma mwanafunzi kwa pasi ya umeme

Tukio hili limetokea  tarehe 20/12/2018 majira ya 19:30hrs ambapo Jeshi la Polisi lilipata taarifa kuwa huko maeneo ya Mtaa wa Lumaliza kata ya Mbugani Manispaa ya Tabora  kijana mmoja aitwaye  JUMANNE NTIMIZI, HUSSEIN, Miaka 17, Mwanafunzi kidato cha tatu katika shule ya sekondari Cheyo, alijeruhiwa na Askari  anayefahamika kwa jina la E.9301 CPL ALMAS   kwa kuchomwa  na pasi ya umeme sehemu mbalimbali za mwili wake na kisha kupigwa na kitu kizito kwenye paji la uso, mdomoni na kumsababishia maumivu makali mwilini.

Chanzo cha tukio hili ni kutokana na  kijana JUMANNE NTIMIZI kukutwa  na bwana ALMAS  akiwa amemkumbatia binti yake aitwaye AMINA ALMASI, Miaka 17, Mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Cheyo karibu na nyumba yake  kwa nia ya kufanya mapenzi ndipo baba mzazi wa Binti huyo alipochukua hatua ya kufanya kitendo hicho kibaya.

Akiongea na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora    ACP – EMMANUEL NLEY amesema  Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora limechukua hatua kwa askari huyo  kwani hadi sasa anashikiliwa  na  uchunguzi ukikamilika atachukuliwa  hatua zaidi za kisheria.

Comments

Popular posts from this blog

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja