Msaidizi wa waziri ashikiliwa kwa tuhuma za kubaka

Kwa kipindi cha wiki moja Jumla  ya makosa matano ya udhalilishaji yameripotiwa katika vituo mbali mbali ndani ya mkoa wa mjini magharib unguja.

Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo kwa waandishi wa Habari  Kamanda wa Jeshi La Polisi mkoa wa Mjini Unguja Thobias Sedoyeka alisema katika Matukio hayo watuhumiwa watatu wamekamatwa akiwemo Shabani Ali Othman miaka 32 Mkaazi wa Mpendae ambaye ni msaidizi binfsi wa waziri.

Alisema Shaban anadaiwa kutenda kosa hilo Novemba 18 mwaka huu saa 10:00 jioni katika ofisi ya serikali, Maruhubi.

Alisema mtuhumiwa anadaiwa kumpa kinywaji mshichana (jina linahifadhiwa) ambae pia ni mfanyakazi mwenzake na kusababisha kupoteza fahamu na hatimae kumbaka.

Alisema uchunguzi bado unaendelea huku taratibu za kumfikisha mahakani mshitakiwa zikiendelea.

Pia alisema jumla ya matukio matatu ya vifo yameripotiwa ambayo yalitokea baina ya Disemba 17 na 21 katika maeneo tofauti ya mkoa huo.

Alisema Disemba 17 saa 10:00 jioni katika pwani ya Maruhubi, Hussein Abdalla Saleh (22) mkaazi wa Chumbuni baada ya kuzama baharini.

Alisema marehemu alikuwa akiogelea na wenzake na mwili wake ulifikishwa hospitali ya Mnazimmoja kwa uchunguzi na kukabidhiwa jamaa zake kwa mazishi.

Aidha tukio jengine lilitotokea Disemba 21 saa 11:00 asubuhi Magomeni ambapo Asha Ali Abeid (55) alikutwa amefariki dunia baada ya kujinyonga.

Pia tukio jengine lilitokea tarehe hiyo hiyo saa 11:00 jioni Mtoni ambapo mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la Nassir alishambuliwa na watu wenye hasira baada ya kutuhumiwa kwa kosa la kuiba.

Comments

Popular posts from this blog

KESI YA ZITTO MUSWADA WA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA YAHAMISHWA

Waziri asimamisha likizo za Marubani ATCL