Bunge lavunjwa kuitisha uchaguzi mpya 2019
Viongozi wa vyama vinavyounda Serikali ya Mseto ya Israel wamekubaliana kulivunja Bunge na kuitisha uchaguzi mpya Aprili 2019.
Baada ya mkutano wa leo Jumanne kwa sauti moja wamekubaliana kuvunja
Bunge na kuitisha uchaguzi mapema baada ya muhula wa miaka minne.
Hatua hiyo imefikiwa huku kukiwa na mvutano ndani ya Serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ya siasa za mlengo wa kulia.
Netanyahu amekabiliwa na shinikizo la madai ya ufisadi, huku waendesha
mashtaka wakimtafutia sababu za kumfungulia mashtaka tokea mwanzoni wa
mwaka.
Hata hivyo, ripoti zinasema kuwa Mkuu wa zamani wa Jeshi la Ulinzi la
Israeli (IDF), Benny Gantz, anajiandaa kugombea kama mgombea binafsi
hali ambayo inaweza kusababisha ugumu wa kutabiri matokeo.
Netanyahu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Likuda amehudumu kama Waziri Mkuu wa Israel tangu 2009 mpaka sasa.
Comments