CCM Morogoro watoa sifa hizi

iNa MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Morogoro kimewataka wananchi wote kumpa moyo Rais Dk. John Magufuli, kwani kazi anayoifanya chini ya serikali yake ni ya kishujaa kwa Watanzania wote.
Pamoja na hali hiyo chama hicho kimewataka wananchi kuzidisha bidii ya kazi na uzalishaji wenye tija kwa manufaa pindi wanapokuwa kwenye ofisi zao, viwandani au mashambani.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Innocent Kalogeresi alisema wananchi, viongozi , wanaharakati  na wanasiasa , wote  wana wajibu wa kutokuwa wepesi kurubuniwa au kununuliwa utu wao kwa kushiriki  usaliti.
“Rais Magufuli ni shujaa wa kweli wa maendeleo katika Taifa letu na kwa hali hii Watanzania wote kwa umoja na mshikamano wetu tumpe ushirikiano wa kila aina.
“Tanzania ni moja na itabaki moja daima kwani  ni miongoni mwa nchi yenye hazina kubwa katika nchi za Kusini mwa Afrika iliohifadhi wapigania uhuru,” alisema Kalogeresi .
Mweyekiti huyo wa CCM alisema mara baada ya uhuru , Taifa limejenga umoja, kuvunja   matabaka ya ukabila, udini,  siasa za ubaguzi wa rangi , ukanda, kulinda  misingi ya   sheria na usawa kwa sauti moja .

“Kwa  kutambua umoja ni nguvu utengano ni udhaifu .Tulijali na kuthamini  sauti  moja .Mwaka 1964 tukaziunganisha Tanganyika na Zanzibar tukaunda Taifa moja ambalo halikuachwa na wakoloni,” alisema
Alisema serikali ya  Tanzania ilijenga viwanda,  kuanzisha mashirika ya umma, kampuni na wakala za serikali , lengo  ni kujijenga kiuchumi ili nchi na watu wake wajitegemee bila kusubiri misaada, fadhila za wahisani.
“Rais Dk Magufuli imepania kurudisha heshima ya nchi  kiuchumi ili tujitegemee kwa  matumizi bora ya rasilimali  , maliasili , maziwa  na bahari .Wananchi tunatakikiwa kufanya kazi kwa bidii na nidhamu ,” alisema

Amefahamisha kuwa malengo ya utekelezaji huo yameanza kwani hivi sasa  kila mtu anatakiwa kutotanguliza itikadi za vyama badala yake wajione wana wajibu wa  kuuunga mkono sera za serikali, mipango na mikakati iliopo.

“Serikali  imekusudia kulinda rasimali za Taifa ili zitumike  kwa maendeleo ya watu. Inahimiza nidhamu ya kazi toka   serikali kuu , halmshauri za wilaya , vyombo vya sheria, wakala za umma , taasisi , wizara na idara za serikali,” alisema mwenyekiti huyo

Akitaja baadhi ya mafanikio yaliopatikana alisema kuondoshwa kwa kero  sugu ya kukosekana madarasa na madawati  shule za msingi,  kutoa elimu ya  msingi hadi kidato cha nne bure huku ikijenga vituo vya afya, wodi za wagonjwa na kina mama wajawazito.

Comments

Popular posts from this blog

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja