Ilichokisema Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) juu ya mafuriko

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari kwa wakazi wa baadhi ya mikoa nchini humo kutokana na vipindi vya mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha katika siku tano zijazo.

Hayo yameelezwa jana Jumapili Desemba 16, 2018 katika  taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na mamlaka hiyo.

TMA imewataka wakazi wa maeneo ya Kanda ya Ziwa, Kaskazini, Kusini na karibu na Bahari ya Hindi kuchukua tahadhali hiyo.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa kuanzia leo Jumatatu Desemba 17, 2018 hadi Desemba 20, 2018 baadhi ya mikoa itaathiriwa na mafuriko jambo ambalo litafanya baadhi ya shughuli za kijamii kusimama.

“Hii inamaanisha kuwa mafuriko yatatokea katika maeneo mengi na kuathiri jamii nzima, kuvurugika kwa usafiri na barabara kubwa kutopitika, hatari kwa maisha kutokana na maji kujaa au yanayopita kwa kasi,” inaeleza.

Comments

Popular posts from this blog

KESI YA ZITTO MUSWADA WA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA YAHAMISHWA

Waziri asimamisha likizo za Marubani ATCL