Fastjet yasitisha safari zake, kurudisha nauli kwa abiria
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Kampuni ya Ndege ya Fastjet Tanzania imesitisha safari zake kwa muda usiojulikana kutokana na sababu za kiutendaji.
Taarifa iliyotolewa na Fastjet leo Jumatatu Desemba 17, kampuni hiyo pia imetoa taarifa kwa wateja wake wote waliokata tiketi kwa ajili ya kusafiri kati ya Desemba mwaka huu na Januari mwakani watarudishiwa fedha zao na Menejimenti ya Fastjet.
“Wateja wote watarudishiwa fedha zao za nauli kwa utaratibu walionunua kuanzia Desemba 20 mwaka huu pia makampuni na mashirika mbalimbali ambayo yalikuwa yanafanya biashara na fastjet yawasiliane nasi kupitia barua pepe au maofisa husika, tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza,” imesema taarifa hiyo.
Comments