Bashir Ngangari agoma kuachia Urais

3 hours ago Comments Off on Bashir Ngangari agoma kuachia Urais
Rais wa Sudan, Omar al-Bashir amekataa wito wa kujiuzulu nafasi ya urais kufuatia maandamano yaliyozuka kumpinga, pamoja na vyama vya upinzani kujiondoa katika makubaliano ya utawala wa mseto.
Chama tawala cha National Congress Party (NCP) kimeeleza kuwa Rais al-Bashir hawezi kujiuzulu. Chama hicho kimesema hatua iliyochukuliwa na vyama vilivyokuwa vinaunda mseto wa utawala ni kinyume cha makubaliano ya majadiliano ya ushirikiano yaliyofikiwa mwaka 2016.
Mwishoni mwa juma lililopita, vyama kadhaa vilitangaza kujiondoa kwenye mseto wa utawala na kujiunga na vyama vingine vya upinzani vinavyoratibu maandamano ya kupinga utawala wa al-Bashir nchini humo.
Msemaji wa NCP, Ibrahim al-Siddiq ametaja hatua hiyo ya vyama vilivyokuwa kwenye ushirika wa madaraka kama, “kujiondoa kwenye muafaka wa kitaifa uliotiliwa saini kwenye nyaraka ya Taifa na ni kinyume cha maadili na taratibu za siasa safi.”
Aliongeza kuwa
al-Bashir ameagiza kuundwa kwa kamati maalum ya kufanya uchunguzi wa vurugu zinazoendelea nchini humo.
Imeelezwa kuwa takriban watu 19 wameuawa na mamia wamejeruhiwa kufuatia maandamano ya kupinga utawala wa al-Bashir yaliyoanza Desemba 19 baada ya Serikali kutangaza ongezeko la bei ya bidhaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na vyakula.


Comments

Popular posts from this blog

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja