Lukuvi, Makonda Wacharukia Migogoro ya Ardhi Gongo la Mboto

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi, yupo Mkoani Dar es Salaam akitatutua kero mbalimbali za wananchi wenye migogoro ya Ardhi , nyumba na masuala mbalimbali yanayohusu uvamizi wa nyumba.

Lukuvi ameanza ziara yake leo katika Wilaya ya Ilala akiambatana na viongozi wa Mkoa akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema na Maafisa Ardhi wa Wilaya ili kuweza kutatua kero zinazohusiana na masuala ya Ardhi na migogoro ya nyumba.
Akiwa katika ziara yake hiyo kwenye viwanja vya Kampala vilivyopo Gongo la Mboto, Makonda amemwelezea Waziri Lukuvi jinsi ambavyo amekuwa akijitahidi kusikiliza kero za wananchi kuhusiana na migogoro ya Ardhi na kuwapatia elimu ya namna ya kumiliki Ardhi kwa kufuata sheria na kuwa na hati miliki ya eneo husika.
Makonda amemhakikishia kuwa migogoro ya Ardhi katika mkoa wa Dar inaweza kupungua kama wananchi watafuta sheria na kanuni za Wizara ya Ardhi kama wakifuata taratibu zote za manunuzi. Kwa upande wake, Lukuvi amewaahidi wananchi kuanza kutoa kero zao na kuanza kuzipatia ufumbuzi hadi jioni hii. Lukuvi yupo Ziarani mkoani Dar es Salaam kwa siku 5 akitatua kero za ardhi zinawazowakabili wananchi mkoani humo.
 
https://youtu.be/G_aoaD7JqgI  to see video

Comments

Popular posts from this blog

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja