Posts

Zuma azua mvutano

Image
4 hours ago Comments Off on Zuma azua mvutano baada ya kupewa msaada wa kurekodi albam yake Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amezua sintofahamu baada ya kupewa msaada na Serikali ya Manispaa kurekodi albam yake ya muziki. Halmashauri ya Manispaa ya Wilaya ya eThekwini kupitia kitengo cha Utamaduni na Urithi imetoa ofa ya kugharamia albam hiyo inayotarajiwa kurekodiwa mwezi Aprili. Albam hiyo inatarajiwa kuwa na nyimbo ambazo zinazungumzia harakati za ukombozi, mapambano kwenye ulingo wa siasa pamoja na maswahibu yaliyowakuta. Chama cha upinzani cha Democratic Alliance kimeeleza kuwa kitamuandikia barua Meneja wa eThekwini kumzuia kutumia fedha za umma kwa ajili ya kufadhili kazi za muziki za Zuma. Diwani wa chama cha Democratic Alliance, Nicole Graham ameeleza kuwa kitengo hicho kilipaswa kutumia fedha hizo kufadhili muziki wa vijana wana

Bashir Ngangari agoma kuachia Urais

Image
3 hours ago Comments Off on Bashir Ngangari agoma kuachia Urais Rais wa Sudan, Omar al-Bashir amekataa wito wa kujiuzulu nafasi ya urais kufuatia maandamano yaliyozuka kumpinga, pamoja na vyama vya upinzani kujiondoa katika makubaliano ya utawala wa mseto. Chama tawala cha National Congress Party (NCP) kimeeleza kuwa Rais al-Bashir hawezi kujiuzulu. Chama hicho kimesema hatua iliyochukuliwa na vyama vilivyokuwa vinaunda mseto wa utawala ni kinyume cha makubaliano ya majadiliano ya ushirikiano yaliyofikiwa mwaka 2016. Mwishoni mwa juma lililopita, vyama kadhaa vilitangaza kujiondoa kwenye mseto wa utawala na kujiunga na vyama vingine vya upinzani vinavyoratibu maandamano ya kupinga utawala wa al-Bashir nchini humo. Msemaji wa NCP, Ibrahim al-Siddiq ametaja hatua hiyo ya vyama vilivyokuwa kwenye ushirika wa madaraka kama, “kujiondoa kwenye muafaka wa kit

Somalia na timuatimua

Serikali ya Somalia imemfukuza nchini humo Balozi wa Umoja wa Mataifa, Nickolas Haysom kwa madai kuwa ameingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo. Taarifa ya kumfukuza Haysom imemtaka kuondoka mara moja na kwamba hatakiwi tena kurejea ndani ya nchi hiyo akidaiwa kuhoji masuala ambayo ni ya ndani ya nchi yanayoleta sintofahamu. Haymon aliandika barua yenye maswali kadhaa kwa Serikali, akiitaka kutoa maelezo kuhusu kuuawa kwa watu waliokuwa wanaandamana kupinga kukamatwa kwa kiongozi wa zamani wa Al Shabaab, Sheikh Muktari Roobow mjini Baidoa, Desemba 13 mwaka jana. Balozi huyo alitaka kufahamu kuhusu hatua na nguvu iliyotumika na kusababisha kuuawa kwa watu 15 katika mvutano wa kumkamata kiongozi huyo. Barua hiyo iliyoelekezwa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi hiyo, ilitaka kufahamu kuhusu ushiriki wa wanajeshi ambao wanaungwa mkono na Umoja wa Mataifa katika kukamatwa kwa Roobow. Alifafanua kuwa, kwa mujibu wa taratibu na mikataba ya kimataifa, usaidizi wa majeshi ya Umoja wa Ma

Siasa safi si kuhama chama

Image
LEONARD MANG’OHA TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) hivi karibuni imemtangaza mgombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Mtolea, kuwa Mbunge wa Temeke, nafasi ambayo alikuwa anaishikilia kipindi akiwa mwanachama wa Chama cha Wananchi -CUF . Tofauti ya ubunge wa sasa na ule aliouvua ni kwamba mara hii amepita bila kupingwa baada ya washindani wake kuondolewa katika kinyang’anyiro hicho kwa kukosa sifa. Kutokana na washindani hao kukosa sifa NEC, imelazimika kumtangaza kuwa mshindi bila hata kwenda katika masanduku ya kupigia kura, na kutoa haki kwa wananchi kumchagua kiongozi wao wanayemtaka. Kitendo cha Mtolea kutangazwa na tume hiyo kushika nafasi hiyo bila kupigiwa kura si cha kushangiliwa si tu na wafuasi wa chama chake kipya bali pia yeye mwenyewe, kitendo hicho kinaondoa dhana ya demokrasia na haki ya kuchagua na kuchaguliwa. Mtolea hapaswi kuufurahia ubunge huo ambao hajautolea jasho. Heshima aliyokuwa nayo awali siamini kama itaend

Mvua ya dakika 45 yazua makubwa

Image
Na IBRAHIM YASSIN-MBOZI MVUA kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha kwa dakika 40 wilayani hapa, imesababisha nyumba 56 kuezuliwa huku watu tisa wakijeruhiwa. Tukio hilo lilitokea katika Kijiji cha Utambalila, Kata ya Nambizo wilayani Mbozi mkoani Songwe. Mbali na maafa hayo, pia mali kadhaa ziliharibiwa. Akizungumza jana na gazeti hili, mmoja wa waathirika hao, Simwinga Mwashambwa alisema alfajiri ya jana walisikia mirindimo na vishindo vikubwa na walipotoka nje walikuta mabati yanapeperushwa na upepo, kuta zikianguka, mazao yaliyotunzwa vyote vikizama majini. Alisema baadaye walitoa taarifa kwa uongozi wa kijiji na kushauriana wakimbilie katika shule ya msingi iliyopo kijijini hapo. “Kwa sasa tunahitaji msaada zaidi ili tuweze kujenga nyumba na kurudi kwenye makazi yetu maana hata mazao tuliyotunza kwa chakula na mbegu yameharibiwa na maji ya mvua, tunahitaji msaada wa haraka,’ ’alisema Mwashambwa huku akitokwa na machozi. Ofisa Mtend

Lukuvi asema haya

Image
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya  Makazi, William Lukuvi, amesema chanzo cha baadhi ya nchi wahisani kugomea kutoa misaada kwa Tanzania kunatokana na msimamo wa Rais Dk. John Magufuli kuhusu kulinda rasilimali za nchi. Kwa mujibu wa Lukuvi msimamo huo haujazifurahisha nchi hizo na kuamua kuweka masharti magumu katika misaada yao kwa Tanzania. Waziri Lukuvi, alitoa kauli hiyo usiku wa kuamkia jana, wakati wa mkesha wa kukaribisha mwaka mpya  wa 2019, uliofanyika Kariakoo, Dar es Salaam ambapo alimwakilisha Rais Magufuli. Waziri Lukuvi, alisema pamoja na hali hiyo, bado Serikali imeendelea kuwa imara na kuhakikisha inakusanya kodi za ndani ili kuweza kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwamo ya umeme wa maji wa Rufiji (Stiegler’s Gorge).   “Leo (jana) tupo kwenye mkesha hapa, hakika nawaomba endeleeni kumwombea kwa dhati Rais Magufuli ili Mungu azidi kumpa nguvu na baraka za kuliongoza Taifa letu. “Mnakumbuka hivi karibuni Tanzania kupitia

Songea kukopesha Wanawake na Vijana kukwama

on Songea yakwama kukopesha Wanawake na Vijan Manispaa ya songea mkoani Ruvuma, imeshindwa kuendelea kukopesha vikundi vya wanawake na vijana kupitia mapatoyake ya ndani, baada ya vikundi hivyo kushindwa kurejesha fedha za mikopo kwa wakati na vinadaiwa zaidi ya sh. milioni 59. Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Tina Sekambo ametoa taarifa katika kikao cha kamati ya ushauri na maendeleo ya mkoa wa Ruvuma (RCC), kuwa vikundi vilivyoshindwa kurejesha mikopo vingi vilikopeshwa katika kipindi cha mwaka 2017/18, na hadi kufika mwezi novemba 2018, na nikikundi kimoja pekee ambacho kimeweza kupunguza deni lake. Katika kipindi hicho cha miaka miwili manispaa hiyo imeweza kuwakopesha wanawake na vijana fedha kupitia makusanyo yeke ya ndani asilimia 10 kila mwezi, ambapo sh. milioni 31.10 zimekopeshwa kwa vikundi vya wanawake, na vijana sh. milioni 28.1. kwa lengo la kupambana na umasikini kwa njia ya ujasiriamali kwa kufanya kazi za mikono, ikiwemo kilimo na biashara ndogo ndogo ili waweze k

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Januari 2, 2019

Image
on Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Januari 2, 2019 Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Januari 2, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.                

Waziri Mkuu atoa ombi kwa Wananchi

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Wananchi kuendelea kushirikiana katika kuibua na kubuni miradi mbalimbali kwa ajili ya kuboresha maendeleo . Waziri Mkuu ameyasema hayo     wakati akipokea msaada wa vyumba viwili vya madarasa vikiwa na  madawati vyenye thamani ya sh. milioni 80 kutoka kwa bank ya CRDB, Kata ya Nachingwea Mkoani Lind i. “Nawaomba wananchi wenzangu tuendelee kushirikiana katika kuibua na kubuni miradi mbalimbali kwa ajili ya kuboresha maendeleo kwenye kata yetu ya Nachingwea.” alisema Majaliwa  Pia Waziri Mkuu alikabidhi kompyuta 20 kwa shule za sekondari tano ambazo ni Kassim Majaliwa, Likunja, Mnacho, Hawa Mchopa na Ruangwa.

VIDEO: Mrisho Gambo kutua na tuzo kwa Rais Magufuli

Image
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amekabidhiwa Tuzo maalum kwa ajili kwenda Rais Magufuli ambapo ni shukrani zao kwa ajili ya kazi nzuri aliyoifanya kwa kipindi cha miaka mtatu tangu aingie madarakani.  PATA MAARIFA ZAIDI

Fahamu faida za Kitunguu Maji mwilini mwako

Image
Kitunguu maji ni aina ya mboga yenye harufu kali inayochangamsha mwili. Pia kitunguu ni kiungo ambacho kina virutubisho katika vyakula na kuvifanya viwe na ladha nzuri. Nchi mashuhuri na maarufu inayolima kiungo hicho ni Misri na kusambaa zaidi duniani na nchini Tanzania kinalimwa zaidi katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Arusha na mikoa mingine ambayo ina rutba nzuri ya kustawisha kiungo hicho. Kiungo hicho kimekuwa kikitibu na kuponya maradhi mbalimbali kutokana na kuwa na salfa ambayo ni nzuri, hasa kwenye ini na husaidia kuponya kansa kwenye utumbo na kinywa kutokana na kuwa na virutubisho vingi vya vitamini C. Kitunguu maji kina kazi nyingi katika mwili wa binaadamu, kwani hutibu magonjwa mbalimbali, ikiwemo kikohozi, vidonda vya tumbo na mifupa, ngozi koo, figo, tumbo na mkojo, kufunga hamu ya kula, hutia kiu na hulainisha tumboni. Pia, kitunguu maji ni chanzo cha madini mengi ambayo yanapatikana katika kiungo hicho ambayo yana umuhimu mkubwa