Waziri Mkuu atoa ombi kwa Wananchi



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Wananchi kuendelea kushirikiana katika kuibua na kubuni miradi mbalimbali kwa ajili ya kuboresha maendeleo .

Waziri Mkuu ameyasema hayo   wakati akipokea msaada wa vyumba viwili vya madarasa vikiwa na  madawati vyenye thamani ya sh. milioni 80 kutoka kwa bank ya CRDB, Kata ya Nachingwea Mkoani Lindi.

“Nawaomba wananchi wenzangu tuendelee kushirikiana katika kuibua na kubuni miradi mbalimbali kwa ajili ya kuboresha maendeleo kwenye kata yetu ya Nachingwea.” alisema Majaliwa 
Pia Waziri Mkuu alikabidhi kompyuta 20 kwa shule za sekondari tano ambazo ni Kassim Majaliwa, Likunja, Mnacho, Hawa Mchopa na Ruangwa.



Comments

Popular posts from this blog

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja