NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Dk. Angelina Mabula amewavua nyadhifa wakuu wa Idara ya Ardhi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kazi ipasavyo. Waliovuliwa nyadhifa hizo ni Mkuu wa Idara ya Ardhi wa Manispaa ya Kigoma, Brown Nziku, Mkuu wa Idara ya Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Emanuel Magembe na Ofisa Ardhi Mteule, Paul Misuzi. Mabula alifanya uamuzi huo Januari 3, mwaka huu akiwa mkoani hapa baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Manispaa ya Kigoma Ujiji na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma. Alifikia uamuzi huo baada ya watendaji hao kushindwa kusimamia maagizo na maelekezo yaliyotolewa tangu mwaka juzi kuhusu ukusanyaji wa kodi ya ardhi, uingizaji wa wamiliki wa viwanja na mashamba kwenye mfumo wa malipo kwa njia ya kielekroniki wa ardhi na utoaji wa hati za madai kwa wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi. Mabula alisema pamoja na barua iliyoandikwa na Kamishna wa Ardhi Msaidiz...
Comments