Songea kukopesha Wanawake na Vijana kukwama
Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Tina Sekambo ametoa taarifa katika kikao cha kamati ya ushauri na maendeleo ya mkoa wa Ruvuma (RCC), kuwa vikundi vilivyoshindwa kurejesha mikopo vingi vilikopeshwa katika kipindi cha mwaka 2017/18, na hadi kufika mwezi novemba 2018, na nikikundi kimoja pekee ambacho kimeweza kupunguza deni lake.
Katika kipindi hicho cha miaka miwili manispaa hiyo imeweza kuwakopesha wanawake na vijana fedha kupitia makusanyo yeke ya ndani asilimia 10 kila mwezi, ambapo sh. milioni 31.10 zimekopeshwa kwa vikundi vya wanawake, na vijana sh. milioni 28.1. kwa lengo la kupambana na umasikini kwa njia ya ujasiriamali kwa kufanya kazi za mikono, ikiwemo kilimo na biashara ndogo ndogo ili waweze kukuza mitaji yao.
Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa tayari manispaa yake imekwisha ingiwa na mashaka juu ya vikundi hivyo kurejesha fedha za mikopo waliyowapa kwa wakati , kwani ni kikundi kimoja tu cha wanawake cha Zikongini ndiyo tayari kimepunguza deni la mkopo wao.
Maofisa wa maendeleo ya jamii manispaa ya Songea tayari wamesha anza kuandaa barua za kuvikumbusha vikundi hivyo kurejesha mikopo yao, ambazo zitapitia kwa maofisa watendaji kata ambao ndio wanaovitambua vikundi hivyo na walithibitisha utambulisho wao kabla ya kuomba mikopo ambayo makubaliano ni kuanza kurejesha baada ya miezi sita ya kwanza.
Kwa upandewake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa RCC, Chiristina Mdeme ameagiza harimashauri zote mkoani hapo kujiwekea utaratibu mzuri wa ukusanyaji wa fedha za mikopo ili ziweze kuwanufaisha wananchi wengine wenye mahitaji ya fedha hizo.
Comments