Posts

JITIBU JIPU KWA DAW HII

Image
Bilinganya ni kiungo ambacho hutumika kuongeza / kuleta ladha katika mboga. Pamoja kuwa ni kiuongo ambacho hutumika kuongeza ladha katika mboga pia Ikumbukwe ya kwamba bilinganya ni tunda ambalo ni dawa, ambapo hutumia kutibu magonjwa yafuatayo; Vidonda vya tumbo. Linasaidia sana kwa watu wenye matatizo ya kukosa usingizi wanashauri kula kwa wingi. Pia kwa wale wenye matatizo ya  homa, Ikumbukwe bilinganya husaidia mtu kuwa na afya nzuri ya mwili pindi atakapolitumia. Kwa wale wenye matatizo ya jipu kumbuka ya kwamba bilinginya ni dawa tosha juu ya tatizo hilo, unachotakiwa kufanya ni kwamba lipondeponde kisha uweke katika jibu. Pia kama utaamua kutengeneza jusi yake, inaaminika ya kwamba tunda hili lina uwezo madhubuti wa kuondoa sumu zote zilizopo mwilini. Endelea kutembelea Muungwana Blog kila wakati ili kupata masomo mengine mengi kama haya kila siku. Asante

HABARI ZA LEO 25/12/2018

Image

Chadema kutembeza bakuli kesi ya mbowe

Image
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeanza kuchangishana fedha kuongeza nguvu ya wanasheria katika kesi zinazowakabili wanachama na viongozi wake wakiwamo Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko. Mbowe na Matiko ambao wanakabiliwa na kesi ya uchochezi inayowakabili pamoja na viongozi wengine saba wa chama hicho, walifutiwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 24 katika ofisi za Chadema Kanda ya Pwani zilizopo Magomeni Makuti, Mwenyekiti wa kanda hiyo, Frederick Sumaye, amesema wanataka haki itendeke haraka ili viongozi hao watoke gerezani waendelee na shughuli zao. “Kanda ya Pwani kwa kuona kwamba mwenyekiti wa taifa yuko ndani tulihitisha mchango wa kusaidia jambo hilo na juzi tulipata Sh 800,000 za kuanzia. “Iringa wanaendelea na michango hiyo na tutandelea kuongeza nguvu ya mawakili. Tunaguswa san

TAARIFA KWA UMMA

Image

Duh! :Baada ya muda mrefu Nape ajitokeza

Image
Jumapili , 23rd Dec , 2018 Na Mwandishi wetu Mbunge wa Mtama na Waziri wa zamani wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ameshindwa kuficha hisia zake juu ya ushindi walioupata timu ya Simba dhidi ya klabu ya Nkana ya Zambia. Nape Nnauye Nkana ambayo ilichuana na Simba leo Jijini Dar es salaam kwenye Uwanja wa Taifa ilishuhudia Simba ikifanikiwa kutinga hatua ya makundi ya michuano klabu bingwa Afrika kwa ushindi wa mabao 3-1. Kupitia ukurasa wake Twitter Nape Nnauye ameandika ameshindwa kujiuzuia moja ya goli lilifungwa na mshambuliaji Clatous Chama na kusema bao hilo ni la aina yake. "Nimejificha vya kutosha, lakini kwa goli hili, Simba hii kiboko This is Simba" aliandika Nape. Watu wengine mashuhuri wakiwemo mastaa wa filamu na muziki wameelezea furaha zao juu ya ushindi wa Simba kama inavyoonekana hapo chini.

'Namshangaa sana Mungu'' - Magufuli

Image
Jumapili , 23rd Dec , 2018 Na Fatuma Muna Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  John Pombe Magufuli amekiri kushangazwa na mambo Mungu anayoitendea Tanzania katiika kipindi hiki. Rais Magufuli akiongea wakati wa kupokea ndege. Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akihutubia katika mapokezi ya ndege aina ya 'Air Bus' A220-300 leo, Disemba 23 jijini Dar es salaam. Amesema kwamba kwa baraka ambazo Mungu amekuwa akiipatia Tanzania ni wazi haitashikika na kwamba mambo yataendelea kunyooka sana. "Nataka niwahakikishie kadiri tunavyoendelea Tanzania haitashikika tutakuwa juu mno. Tanzania tunaweza na tutaweza. Mambo yananyooka mno mpaka mimi namshangaa Mungu. Mungu anatupenda na yupo pamoja na sisi", - amesema. Pamoja na hayo, Rais Magufuli amesema kwamba 'Air Bus' ni dege ya kwanza katika nch

Mizengo Pinda kuutaka Urais?

Image
Jumapili , 23rd Dec , 2018 Na Mwandishi wetu Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda amewajibu watu ambao wamekuwa wakimhoji juu ya kuhitaji nafasi ya Urais 2020 kuwa rais wa sasa John Magufuli ndiye kiongozi ambaye anafaa kwa sasa kuiongoza Tanzania. Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda . Pinda ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Dodoma ambapo amesema wakati fulani kwenye uongozi wake wapinzani waliwahi kusema serikali yao ni dhaifu haina makali hivyo walikuwa wanataka kiongozi mkali na mwenye uthubutu. " Wakati fulani kuna baadhi ya watu huwa wananiuliza hivi mzee na wewe si ulikuwa unautaka urais nawajibu tu aka huyu huyu ndiye anayefaa, mimi ni miongoni mwa watu wanaomkubali sana JPM ." amesema. Amesema chini

Kodi: Makonda kimya kosa!

Image
Jumapili , 23rd Dec , 2018 Na Mwandishi wetu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewaasa wananchi wa Dar es salaam kujenga tabia ya kulipa kodi, ili kuhakikisha serikali inatekeleza miradi ya Maendeleo nchini huku akimwahidi Rais kuwa atakuwa kimya akitengeneza mpango wezeshi kwa walipa kodi. Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda. Makonda ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es salaam, wakati wa hafla ya upokeaji wa ndege ya mali ya Shirika la Ndege la Tanzania aina ya Airbuss A220-300 ambayo imefanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere. " Niwaombe wananchi tumuunge mkono Rais wetu juu ya kulipa kodi Mheshimiwa Rais baada ya Krismas mimi na RAS wangu tutakuwa kimya kwa ajili ya kuja na mfumo mzuri wa kulipa kodi ." Ameongeza Makonda. Makonda amesema " Mheshimiwa Rais tu

Mizengo Pinda azungumzia maumivu ya Upinzani

Image
Jumatatu , 24th Dec , 2018 Na Mwandishi wetu Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda ameweka wazi jinsi alivyokuwa akiumizwa na kauli za upinzani dhidi ya uongozi wake na kusema kuwa anaushangaa upinzani kulalamikia uongozi amabo waliulilia kwa muda mrefu. Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda. Akifungua Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dodoma, Pinda amesema kuna kipindi wakati wa uongozi wake, wapinzani walikuwa wakiinyooshea kidole serikali yao kuwa ni dhaifu haina makali, hivyo walikuwa wanataka kiongozi mkali na mwenye uamuzi mgumu. " Kauli hiyo na ilikuwa ikinikera kwa sababu ilitulenga viongozi wa wakati ule, lakini sasa nashangaa kuona wapinzani haohao wameanza kulalamika tena juu ya utendaji kazi wa Rais John Magufuli ambaye ndiye kiongozi wa aina waliyekuwa wakitama

Vigogo 29 Krismasi yawa chungu kwao

Image
MWANDISHI WETU – Dar es Salaam WAKATI keshokutwa Wakristo wote duniani wataadhimisha Sikukuu ya Krismasi na wiki ijayo Mwaka Mpya wa 2019, vigogo 29 watasherehekea wakiwa mahabusu katika magereza mbalimbali nchini. Vigogo hao ni wale wanaoshtakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakituhumiwa kwa kesi mbalimbali, zikiwamo za uhujumu uchumi, biashara ya dawa za kulevya na meno ya tembo. Miongoni mwa vigogo hao ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko. Mbowe na Matiko watasherehekea Krismasi na Mwaka Mpya gerezani baada ya kufutiwa dhamana zao katika kesi ya uchochezi inayowakabili pamoja na wengine saba wa chama hicho. Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea Januari 3, mwakani ikiwajumuisha washtakiwa wengine; Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji, Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Sa

DRC:Wagombea waumana kumrithi Rais Kabila

Image
Markus Mpangala MACHO na masikio ya wadau mbalimbali wa kisiasa yanaelekezwa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambako wananchi wa Taifa hilo wanatarajia kufanya Uchaguzi Mkuu. Awali Tume ya uchaguzi nchini humo, CENI ilitangaza kuwa uchaguzi ungefanyika Desemba 23, mwaka huu, kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya taratibu vikiwemo vifaa kutofikishwa vituoni pamoja na ghala za Tume hiyo kuungua moto mjini Kinshasa uchaguzi huo umeahirishwa hadi Desemba 30, mwaka huu. Takriban wapigakura milioni 46 waliojiandikisha wanatarajia kushiriki zoezi la kuwapigia kura wagombea 34, 900 katika viti 500 vya kitaifa, viti 715 vya mikoa na 21 vya urais na vituo 21,100 vya kupigia kura nchini kote. CENI ilikuwa na mpango wa kusambaza vifaa vya eletroniki 105,000 kutoka kwa kampuni ya Miru Systems ya nchini Korea kusini. Vifaa vingine vinavyopangwa kutumika ni vile vilivyowahi kutumiwa nchini Ubelgiji, Brazil, India, Namibia na Venezuela. Hii

JPM aibua mapya haya

Image
Bethsheba Wambura, Dar es Salaam Rais Dk John Magufuli amebaini siri ya watendaji 100 wa serikali waliokwepa kusafiri ilihali wamekatiwa tiketi za ndege na serikali na amemuagiza Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege nchini (ATCL) kufikia kesho awe amempelekea majina yao ili wakatwe mishahara yao kufidia tiketi hizo. Akizungumza wakati kuipokea ndege mpya aina ya Airbus A220-300, leo Jumapili Desemba 23, katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam Rais Magufuli amesema imekuwepo tabia ya watendaji wa serikali kusitisha safari zao bila kutoa taarifa yoyote ilihali wameshakatiwa tiketi tayari. Rais Magufuli amesema hali hiyo ni kero hata kwa abiria wengine kwani wanafika uwanjani wanaambiwa ndege imejaa kumbe haijajaa ila kuna watu walikatiwa tiketi na hawakusafiri. “Watu wanakatiwa tiketi ila hawasafiri wanakaa kimya hadi muda wa safari unafika ndege iko tupu na inaondoka hivyo hivyo. “Kuf

kilichomtokea Haji Manara Baada ya ushindi wa Simba, hiki hapa

Image
Ofisa habari wa Simba, Haji Manara jana alitokwa na machozi ya furaha baada ya kufanikiwa kupindua meza kibabe kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Nkana FC ya Zambia na kuwashukuru mashabiki kujitokeza kuipa sapoti. Simba walifanikiwa kushinda kwa mabao 3-1 uwanja wa nyumbani na kufanikiwa kushinda kwa jumla ya mabao 4-3 baada ya matokeo ya awali Simba kukubali kichapo cha mabao 2-1. Manara amesema kuwa walijipanga na waliwaambia mashabiki wao wajitokeze kwa wingi uwanja wa Taifa ili kuwapa morali wachezaji kupambana na ndivyo ilivyotokea. "Ujinga huwa unakuwa wakati wa kwenda tu wakati wa kurudi hakuna kitu kama hicho, tunawashukuru mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi na sapoti yao waliyotoa hatimaye yametia," alisema.

Meru wazee 264 wapatiwa Bima ya Afya

Image
Na Alphonce Kusaga Arusha. Wazee 264 katika Wilaya ya Meru mkoani Arusha wamepatiwa kadi za bima ya afya zitakazowawezesha kupata huduma za afya katika vituo mbali mbali vya afya hivyo kuboresha ustawi wa maisha ya wazee. Akikabidhi Bima hizo kwa wazee  wanaohudumiwa na kituo cha Huduma ya Wazee Sakila kilichopo   wilayani hapo ,Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Meru Elizabeth Mohere alisema kuwa kadi hizo zitawawezesha kupata matibabu kwa mwaka mzima kwa gharama nafuu. Elizabeth Alisema kuwa kuna uhitaji mkubwa wa kuwekeza kwenye afya za wazee kwani ni kundi muhimu katika jamii ambalo linapaswa kupawa kipaumbele kwenye huduma za kijamii. "Ni muhimu kutunza kadi hizi muweze kufika nazo na kupewa matibabu ,tunawashukuru wadau kwa kujitoa kuhudumia wazee kwani serikali haiwezi kufanya kila kitu" Alisema Mratibu wa kituo  cha huduma ya wazee sakila,Hamphrey Mafie alisema kuwa wazee hao wanapaswa kutunza kadi hizo zitazowawezesha kupata huduma

MAGAZETI YA LEO 24/12/2018

Image
Powered by Blogger