Markus Mpangala MACHO na masikio ya wadau mbalimbali wa kisiasa yanaelekezwa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambako wananchi wa Taifa hilo wanatarajia kufanya Uchaguzi Mkuu. Awali Tume ya uchaguzi nchini humo, CENI ilitangaza kuwa uchaguzi ungefanyika Desemba 23, mwaka huu, kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya taratibu vikiwemo vifaa kutofikishwa vituoni pamoja na ghala za Tume hiyo kuungua moto mjini Kinshasa uchaguzi huo umeahirishwa hadi Desemba 30, mwaka huu. Takriban wapigakura milioni 46 waliojiandikisha wanatarajia kushiriki zoezi la kuwapigia kura wagombea 34, 900 katika viti 500 vya kitaifa, viti 715 vya mikoa na 21 vya urais na vituo 21,100 vya kupigia kura nchini kote. CENI ilikuwa na mpango wa kusambaza vifaa vya eletroniki 105,000 kutoka kwa kampuni ya Miru Systems ya nchini Korea kusini. Vifaa vingine vinavyopangwa kutumika ni vile vilivyowahi kutumiwa nchini Ubelgiji, Brazil, India, Namibia na Venezuela. Hii ...
Comments