Ofisa habari wa Simba, Haji Manara jana alitokwa na machozi ya furaha
baada ya kufanikiwa kupindua meza kibabe kwenye mchezo wa Ligi ya
Mabingwa dhidi ya Nkana FC ya Zambia na kuwashukuru mashabiki kujitokeza
kuipa sapoti.
Simba walifanikiwa kushinda kwa mabao 3-1 uwanja wa nyumbani na
kufanikiwa kushinda kwa jumla ya mabao 4-3 baada ya matokeo ya awali
Simba kukubali kichapo cha mabao 2-1.
Manara amesema kuwa walijipanga na waliwaambia mashabiki wao wajitokeze
kwa wingi uwanja wa Taifa ili kuwapa morali wachezaji kupambana na
ndivyo ilivyotokea.
"Ujinga huwa unakuwa wakati wa kwenda tu wakati wa kurudi hakuna kitu
kama hicho, tunawashukuru mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi na sapoti
yao waliyotoa hatimaye yametia," alisema.
Comments