Meru wazee 264 wapatiwa Bima ya Afya
Na Alphonce Kusaga Arusha.
Wazee 264 katika Wilaya ya Meru mkoani Arusha wamepatiwa kadi za bima ya afya zitakazowawezesha kupata huduma za afya katika vituo mbali mbali vya afya hivyo kuboresha ustawi wa maisha ya wazee.
Akikabidhi Bima hizo kwa wazee wanaohudumiwa na kituo cha Huduma ya Wazee Sakila kilichopo wilayani hapo ,Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Meru Elizabeth Mohere alisema kuwa kadi hizo zitawawezesha kupata matibabu kwa mwaka mzima kwa gharama nafuu.
Elizabeth Alisema kuwa kuna uhitaji mkubwa wa kuwekeza kwenye afya za wazee kwani ni kundi muhimu katika jamii ambalo linapaswa kupawa kipaumbele kwenye huduma za kijamii.
"Ni muhimu kutunza kadi hizi muweze kufika nazo na kupewa matibabu ,tunawashukuru wadau kwa kujitoa kuhudumia wazee kwani serikali haiwezi kufanya kila kitu" Alisema
Mratibu wa kituo cha huduma ya wazee sakila,Hamphrey Mafie alisema kuwa wazee hao wanapaswa kutunza kadi hizo zitazowawezesha kupata huduma za afya bure bila kulipia .
Mafie anaeleza kuwa shirika la Dorcas International limewawezesha wazee kupata bima za matibabu pamoja na zawadi za sikukuu za krismas na Mwaka mpaya ambapo wazee walipatiwa chakula,mavazi pamoja na mahitaji mengine .
Kwa Upande wake Mzee anayehudumiwa na kituo hicho Maria Solomon ameishukuru kituo hicho kwa kuwajali na kuwathamini kwani wazee hao walikua na changamoto ya matibabu kutokana na uwezo mdogo wa kifedha hivyo watapata fursa ya kutibiwa.
Comments