Kodi: Makonda kimya kosa!

Jumapili , 23rd Dec , 2018
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewaasa wananchi wa Dar es salaam kujenga tabia ya kulipa kodi, ili kuhakikisha serikali inatekeleza miradi ya Maendeleo nchini huku akimwahidi Rais kuwa atakuwa kimya akitengeneza mpango wezeshi kwa walipa kodi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.
Makonda ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es salaam, wakati wa hafla ya upokeaji wa ndege ya mali ya Shirika la Ndege la Tanzania aina ya Airbuss A220-300 ambayo imefanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
"Niwaombe wananchi tumuunge mkono Rais wetu juu ya kulipa kodi Mheshimiwa Rais baada ya Krismas mimi na RAS wangu tutakuwa kimya kwa ajili ya kuja na mfumo mzuri wa kulipa kodi." Ameongeza Makonda.
Makonda amesema "Mheshimiwa Rais tunaweza kukuunga mkono sisi wenyewe kuwa walipa kodi waaminifu, maneno yote haya viongozi wako tukiyasema bila kulipa kodi hatutaweza kufika, kama kuna mambo hayajatimia niwaombe wananchi sasa ni wakati muafaka wa kulipa kodi, kwa sababu tunaona matunda ya ulipaji kodi."
Mamia ya wananchi waishio Dar es salaam na baadhi ya viongozi wa kitaifa wamejitokeza kushiriki hafla hiyo ya kupokea ndege hiyo ambapo.

Comments

Popular posts from this blog

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja