Chadema kutembeza bakuli kesi ya mbowe
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeanza kuchangishana fedha kuongeza nguvu ya wanasheria katika kesi zinazowakabili wanachama na viongozi wake wakiwamo Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko.Mbowe na Matiko ambao wanakabiliwa na kesi ya uchochezi inayowakabili pamoja na viongozi wengine saba wa chama hicho, walifutiwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 24 katika ofisi za Chadema Kanda ya Pwani zilizopo Magomeni Makuti, Mwenyekiti wa kanda hiyo, Frederick Sumaye, amesema wanataka haki itendeke haraka ili viongozi hao watoke gerezani waendelee na shughuli zao.
“Kanda ya Pwani kwa kuona kwamba mwenyekiti wa taifa yuko ndani tulihitisha mchango wa kusaidia jambo hilo na juzi tulipata Sh 800,000 za kuanzia.
“Iringa wanaendelea na michango hiyo na tutandelea kuongeza nguvu ya mawakili. Tunaguswa sana na matatizo yanayotupata na tunaendelea kushiri”amesema Sumaye
Comments