Ndege aina ya AirBus yatua Leo nchini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli leo anatarajiwa kuongoza mamia ya watanzania kupokea ndege ya kwanza kati ya ndege mbili aina ya Air-Bus A220 zilizonunuliwa na serikali ya Tanzania ambayo itawasili leo. Ndege hiyo itawasili leo majira ya saa 8:30 mchana na kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Kwa mujibu wa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria ambaye pia anahudumia nchini Ghana Muhidin Mboweto amesema ndege hiyo ilitua salama Mjini Accra Ghana na kuwa gumzo kwa kila aliyeiona ikiwa uwanja wa ndege. Tukio la kupokea ndege hiyo litafanyika Uwanja wa ndege Mwalimu Julius Nyerere ambapo viongozi wengine mbalimbali wa nchi watawasili kushuhudia tukio hilo. Ndege hiyo A220 iliondoka Montreal Canada juzi saa 1:00 Jioni kwa saa za Canada na ikatua visiwa vya Santa Maria saa 5:00 usiku kwa saa za huko. Mkurugenzi Mkuu wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi ndiye anayeongoza safari ya ndege hiyo kut...