Watu 11 wa familia moja wanusurika kufa kisa kunywa togwa

Picha ya mtandao
Watu 11 wa familia moja wa kijiji cha Mtwarapachani, Namtumbo mkoani Ruvuma, wamenusurika kifo baada ya kunywa pombe aina ya togwa.

Wanafamilia hao kwa sasa wamelazwa katika Kituo cha Afya cha Namtumbo kwa  matibabu, Waliolazwa ni Tatu Ndumbaro (48), Maisha Ndumbaro (14), Issa Ndumbaro (5), Mariamu Issa Ndumbaro (48), Daima Ndumbaro (29) na Khadija Ndumbaro (12).

Wengine ni Asha Omari (80), Asheri Uega (31), Safiruna Omari (32), Matokeo Ndumbaro (13) na Bahati Ndumbaro(25) ambao wote ni wa familia moja ya Ndumbaro walioko katika kijiji hicho.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Dk. Yuna Hamisi, alikiri kuwapo kwa wagonjwa hao katika kituo hicho cha afya na kwamba timu ya madaktari ikiongozwa na Godwin Luta iko kituoni hapo kuhakikisha wanaokoa maisha yao.

Mganga aliyeshiriki katika uchunguzi huo, Dk. Luta, alisema baada ya kuwachunguza wagonjwa hao walibaini ugonjwa huo wa kutapika na kuharisha ulisababishwa na kitu walichokula katika familia hiyo.

Kwa upande wao, wagonjwa wote walipohojiwa walisema chanzo cha tatizo hilo ni kunywa togwa iliyotengenezwa nyumbani.

Walisema pombe hiyo ilitengenezwa maalum kwa ajili ya kuwakumbuka marehemu katika familia yao na kwamba togwa huandaliwa na chakula huandaliwa kwa ajili ya watu kula.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Asha Omari alisema togwa hiyo ilikuwa imeanza kuharibika na haikunywewa na watu wengi kwa kuwa  baadhi waligundua mapema.

Comments

Popular posts from this blog

KESI YA ZITTO MUSWADA WA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA YAHAMISHWA

Waziri asimamisha likizo za Marubani ATCL