FastJet yaanza kurudisha nauli za abiria
Msemaji wa shirika hilo, Lucy Mbogoro, amesema baadhi ya wateja wao walianza kurudishiwa fedha hizo Jumatatu wiki hii hasa kwa wateja walionunua tiketi kwa njia ya mtandao.
“Jumatatu tulitoa tangazo kuwa tutaanza kushughulikia malipo ya wateja wetu pamoja na wadau wengine tunaofanya nao biashara, siku hiyo hiyo tulianza kushughulikia kwa wale walionunua kwa M-Pesa, Airtel Money na Tigo Pesa.
“Ila kwa wale walionunua kwa ‘cash’ tulitangaza tutaanza kushughulikia malipo yao tarehe 20 na tayari tumeanza kulishughulikia hilo , tumekuwa tukiendelea na taratibu za benki kwa sababu hatuwezi kukaa na fedha nyingi, lazima tuzipeleke benk” amesema Lucy.
Amesema katika urejeshaji wa fedha hizo, watatoa kipaumbele kwa wateja waliotarajia kusafiri kuanzia Desemba 20, hadi 31, mwaka huu ili kuwawezesha kuendelea na shughuli zao, huku wale wanaotarajiwa kusafiri kuanzia Januari, wakiendelea kulipwa taratibu.
Comments