Afariki baada ya kujirusha kutoka ghorofa ya tatu

Jengo la Rock City Mall
Mwanaume mmoja aitwaye Musa Ally mwenye umri wa miaka 25, ambaye ni mkazi wa  mtaa wa Kiloleli wilayani Ilemela jijini Mwanza, amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka gorofa ya 3 hadi chini katika jengo la Rocky City Mall.

Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Advera Bulimba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo leo Desemba 21, majira ya saa 7:00 mchana.

Kamanda amesema kuwa kijana huyo alikuwa amekuwa akilewa kupitiliza na ambapo Desemba 16, 2018 alikamatwa na kuwekwa kituo cha polisi Kirumba, kutokana na kulewa hadi kilevi kilipopungua ndipo akaachiwa huru.

“Baada ya uchunguzi tumebaini kuwa kijana huyo amekuwa akilewa na kuwaambia watu kuwa yeye ni masikini na hana ajira hivyo asilaumiwe mtu yeyote kwakuwa hana wazazi hivyo uamzi huo amechukua yeye mwenyewe'', amesema Bulimba.

Kamanda pia amesema kuwa wamekuta ujumbe ndani ya mfuko wa marehemu ambao unaeleza kuwa ana Shahada Sayansi ya kompyuta aliyoipata Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).

Comments

Popular posts from this blog

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja