Mapya Yaibuka, Aliyedaiwa Kufia Mwananyamala na Dawa za Kulevya Tumboni


KAMISHNA Mkuu Wa Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Siyanga, amesema uchunguzi waliyoufanyika wamebaini kuwa mwili wa mfanyabiashara, Happy Mboya (38) aliyefariki dunia katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam haukuwa na dawa za kulevya kama ilivyoripotiwa awali.
Happy aliyefariki dunia Jumapili iliyopita Desemba 16, 2018 na mwili wake kupangwa kusafirishwa jana kwenda Moshi kwa mazishi, Polisi wa Kituo cha Oysterbay waliuchukua kwa ajili kuupeleka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi zaidi baada ya kudaiwa kuwa ulikuwa na madawa ya kulevya tumboni.
Siyanga amesema maofisa wa Mamlaka hiyo walikuwepo wakati mwili wa marehemu Happy ukifanyiwa upasuaji na haukukutwa na dawa za kulevya kama ilivyodaiwa. Jana Siyanga alisema baada ya uchunguzi huo angetoa taarifa kamili juu ya tukio hilo.

Baba mdogo wa marehemu, Ally Bilali jana alisema baada ya kurejea nchini, Happy alifikia katika nyumba ya kulala wageni ambayo haikufahamika na mtu mwingine isipokuwa mume wake ambapo hata dada yake alikuwa hafahamu kuwa amesharudi kwa sababu alidai kuwa simu yake imeharibika na wasingeweza kuwasiliana kumbe ilikuwa kumficha.

Dada yake huyo alipata taarifa baada ya mdogo wake kuzidiwa na wahudumu kumpigia simu ndipo alienda kumchukua kumuwahisha hospitalini, na baada ya kupimwa, alionekana kuwa na njaa kali jambo ambalo lilimlazimu daktari kumuandikia dripu za maji ili kumsaidia, lakini fariki akiendelea kutibiwa. Mwili wa Happy umeagwa leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

Comments

Popular posts from this blog

KESI YA ZITTO MUSWADA WA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA YAHAMISHWA

Waziri asimamisha likizo za Marubani ATCL