Magufuli ataka jina libadilishwe
Alhamisi , 20th Dec , 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ameitaka mamlaka inayosimamia ujenzi wa wa Daraja la Selander kubadilisha jina hilo na kutoliita kwa jina la mtu, badala yake wanapaswa kubuni jina ambalo litaitangaza Tanzania. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli Akizungumza katika uzinduzi wa uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa daraja hilo, Dk. Magufuli amesema kwamba jina la daraja hilo linapaswa kutangaza nchi haswa ikizingatiwa kuwa daraja hilo lipo maeneo ya ubalozi wa mataifa mbalimbali hivyo itakuwa rahisi kwao kusafiri kwa haraka. " Hili jina la daraja 'New Selander Bridge', nafikiri mngelibadilisha na kuliita jina lingine ambalo litaitangaza Tanzania vizuri kimataifa. Hata mngeliita Tanzanite, kwani ni madini pekee yanayopatikana Tanzania ila msiite jina la mtu ". Pamoja na hayo Rais Magufuli ameongeza kwamba " Mwalimu Ny...