Tundu Lissu anyoosha maelezo kuhusu kugombea Urais 2020
Mwanasiasa wa upinzani nchini, Tundu Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki amesisitiza kuwa iwapo chama chake kitamteua kuwa mgombe wa urasi 2020 yupo tayari. Mwanasheria huyo Mkuu wa CHADEMA akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya BBC amesema yeye kugombea au kutogombea inategemea na maamuzi kutoka kwenye vikao vya chama chake. "Nimesema na ninaomba nirudie tena, kama chama changu na vyama tunavyoshirikiana navyo na Watanzania wanaotuunga mkono watasema kwamba mimi ninafaa, nipo tayari kufanya hivyo," amesema Tundu Lissu. Kwa sasa Tundu Lissu yupo katika ziara nchini Uingereza, moja ya lengo la ziara yake hiyo ni kueleza tukio la kushambuliwa na kujeruhiwa vibaya kwa risasi Septemba 17, 2017.