Posts
Ubungo yapata neema hii
- Get link
- X
- Other Apps
By
Maguruacademy
-
Na ANDREW MSECHU-DAR ES SALAA KITUO kikubwa cha biashara cha kimataifa kinatarajiwa kujengwa katika eneo la Stendi ya Mabasi ya Ubungo, ujenzi utakaoanza Januari mwakani na kuchukua miezi 18 kukamilika. Akizungumza na MTANZANIA jana, Meneja wa Mauzo wa Kampuni ya East Africa Commercial & Logistics Center Tom Zhang, alisema kitakapokamilika kituo hicho kinatarajiwa kuwa namba moja kwa nchi za Afrika Mashariki. Alisema kwa sasa tayari wana vituo viwili vya aina hiyo, cha kwanza kikiitwa Dragon Mall ambacho kipo nchini Dubai na kingine kikiitwa Yiwu City Mall nchini China. “Kituo hiki kitakuwa maalumu kwa ajili ya kuingiza bidhaa kutoka nje na kuuza bidhaa kwenda nje. Kutakuwa karibu na kila kitu kinachohitajika kwa ajili ya biashara za kimataifa. “Hii ina maana kwamba kikishakamilika, hakutakuwa na sababu ya mfanyabiashara wa Tanzania kusafiri kwenda China au nje ya nchi kununua bidhaa na kuzileta nchini. Safari hizo zinagharimu muda mwingi na gharama kub...
LOOOOH! :Simbachawene ampiga mfanyabiashara
- Get link
- X
- Other Apps
By
Maguruacademy
-
Na MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM WAZIRI wa zamani wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene, ameingia matatani baada ya kudaiwa kumshambulia mkazi wa Magomeni, Dar es Salaam, Kassim Abdallah (37) hadi kusababisha alazwe Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Simbachawene ambaye pia ni Mbunge wa Kibakwe (CCM), anadaiwa kutenda tukio hilo Jumatatu wiki hii eneo la Vingunguti, wilayani Ilala. Abdallah ambaye ni dereva, hivi sasa amelazwa Muhimbili akipatiwa matibabu ya majeraha. Aliumia kichwani na sehemu nyingine za mwili. Akizungumza na MTANZANIA juzi, Abdallah aliyelazwa wodi namba 18 ya wagonjwa binafsi kwenye jengo la Sewahaji, alisema alikumbwa na mkasa huo Jumatatu usiku alipokuwa katika harakati za kwenda kuegesha gari ofisini kwao. Dereva huyo alikuwa akitoka safarini Rwanda na alisema ‘yard’ yao iko jirani na baa ya Titanic mahali ambako tukio lilitokea. “Ilikuwa saa 6 usiku, nilikuwa nakwenda kuegesha...
Duh!: Mchezaji huyu apatwa na haya
- Get link
- X
- Other Apps
By
Maguruacademy
-
Huyu mama aamua kusema!
- Get link
- X
- Other Apps
By
Maguruacademy
-
Mchungaji wa Kanisa la Assemblies Of God maarufu kama ‘Mlima wa moto’ Dk Getrude Rwakatare, amemshukuru Rais Magufuli kwa kumgundua Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam. Mama Rwakatare amesema kuwa kwa mara ya kwanza alimuona Makonda ana bidii ya tofauti na jasiri. "Namshukuru Rais wetu kwa kumgundua Paul Makonda , mimi nakumbuka nilikumgundua akiwa kiongozi wa Wana vyuo pale Moshi alivyonialika kwenye mkutano mkubwa kabisa wa wana vyuo," alisema Mama Rwakatare. "Nilimuona ana bidii ya tofauti na ujasiri wa tofauti, niliona kwamba Mungu amempa wito ndani yake, nilikuiwa nasema Mungu naomba utokee mahali fulani kiwa bahati tukakutana tena kwenye Bunge la Katiba." Mama Rwakatare ameyasema hayo katika hafla ya viongozi wa dini iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda ya kupata chakula cha pamoja.
Kigogo mwendokasi, wenzake waachiwa kwa dhamana
- Get link
- X
- Other Apps
By
Maguruacademy
-
Na MWANDIDHI WETU – DAR ES SALAAM WAFANYAKAZI saba wa Kampuni ya Uda-Rapid Transit (UDART), akiwamo kigogo wa idara ya fedha, wanaodaiwa kuhusika katika mtandao wa uhujumu wa mapato ya mabasi ya mwendokasi kwa kuchapisha tiketi feki kwa abiria wameachiwa kwa dhamana. Hatua hiyo imekuja baada ya kushikiliwa kwa zaidi ya siku 60 na Jeshi la Polisi huku wakiendelea kusubiri uamuzi wa jalada lao ambalo lipo kwa mwanasheria mkuu wa Serikali, likisubiri hatima yao kama kufikishwa mahakama ama laa. Pamoja na kuachiwa, wafanyakazi hao ambao awali walikuwa wanane wametakiwa kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi mara kwa mara huku upelelezi wa kesi yao ukiendelea. Akizungumza na MTANZANIA jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alisema tuhuma zinazowakabili wafanyakazi hao ni za kughushi na kuhujumu mapato ya mradi wa mabasi ya mwendokasi, hivyo upelelezi wake unachukua muda mrefu ili kuhakikisha wanapata mtandao mzima. Alise...
Aliyetekwa kwa miaka 30 apatikana
- Get link
- X
- Other Apps
By
Maguruacademy
-
Alhamisi , 27th Dec , 2018 Na Mwandishi wetu Mwanamke mmoja raia wa Argentina ameokolewa na polisi baada ya kushikiliwa mateka kwa zaidi ya miaka 30. Mwanamke aliyeokolewa na polisi baada ya kushikiliwa mateka kwa miaka 30 (wapili kushoto) na mwanae wa miaka tisa wameungana na familia yao. Operesheni ya kumnasua mwanamke huyo ilifanyika kwa ushirikiano wa polisi wa nchi za Argentina na Bolivia. Mahala ambapo alikuwa akishikiliwa mwanamke huyo ambaye sasa ana umri wa miaka 45 lilikuwa halifahamiki toka miaka ya 80. Hata hivyo, mapema mwaka huu, polisi walipata taarifa kuwa alikuwa akishikiliwa katika eneo la Bermejo, kusini mwa Bolivia baada ya uchunguzi, polisi walifanikiwa kuitambua nyumba aliyokuwemo na kufanikiwa kumuokoa akiwa na mtoto wake mwenye umri wa miaka tisa. Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji katika taarifa iliyotolewa na polisi nchini Argentina wanasema mwanamke huyo amefanikiwa kurejeshwa na kuungana na...
Krismasi yawa hatari Kagera
- Get link
- X
- Other Apps
By
Maguruacademy
-
Alhamisi , 27th Dec , 2018 Na Mwandishi wetu Watu wanne wamefariki dunia mkoani Kagera katika kusherehekea sikukuu za Krismasi na siku ya Boxing Day , kufuatia matukio manne yaliyotokea kwa nyakati tofauti mkoani humo. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Revocatus Malimi, lipo tukio la Desemba 25 katika kijiji cha Kigorogoro wilaya ya Kyerwa, mwanamke alipigwa na mpenzi wake wakati wakisherehekea sikukuu hiyo kwenye moja ya majumba ya starehe, ambapo mwanaume huyo alimtuhumu mpenzi wake kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine. Katika tukio la pili Kamanda huyo amesema kuwa Justus Clemence mwenye umri wa miaka 42 mkazi wa kitongoji cha Itokozi wilayani Biharamulo anayedaiwa kuwa na ugonjwa wa akili, alipoteza maisha baada ya kupigwa na watu waliomtuhumu kuiba kondoo wa mwanakijiji mwenz...
UVCCM wampitisha mgombea Urais CCM 2020
- Get link
- X
- Other Apps
By
Maguruacademy
-
Alhamisi , 27th Dec , 2018 Na Mwandishi wetu Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, kupitia kwa Katibu wa idara ya uhamasishaji na chipukizi Hassan Bomboko, imesema kuelekea uchaguzi wa mwaka 2020 umoja huo utaenda Dodoma kuhakikisha Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wa sasa Rais John Pombe Magufuli, anapewa Umoja wa Viajana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM wakiwa kwenye kikao. nafasi ya kuwania tena Urais. Kwa mujibu wa Bomboko kwenye kikao kitakachofanyka Dodoma Umoja huo hautakuwa na lengo jingine zaidi ya kumpitisha Rais Magufuli kuwania tena nafasi hiyo ya kukiongoza chama hicho kwenye uchaguzi wa awamu ya pili. " Kama msemaji rasmi wa UVCCM, msimamo wa taasisi yetu ni kwamba hatuna na hatutakuwa na mchakato wa kumtafuta mgombea Urais 2020 mwingine zaidi ya Magufuli ambaye ndiyo Mwenyeki...
VIDEO: Walalamikia hali kibiashara kuwa ngumu
- Get link
- X
- Other Apps
By
Maguruacademy
-
Wafanyabiashara wa maduka katika stendi ndogo jijini Arusha wamefunguka na kuelezea hali ya kibiashara katika kipindi hiki cha sikukuu ya krismas na mwaka mpya kwamba ni ngumu kuliko mika iliyopita ilikuwa na afadhali. Akizungumza Katibu wa wafanyabiashara stendi ndogo jijini Arusha Anjelo Shokia amesema kuwa kwa hali hiyo itapelekea wengi kufunga biashara na kutafuta vitambulisho ili kurudi hali ya kuwa wamachinga.
VIDEO: Maalim Seif kutua ACT Wazalendo siri yafichuka, CUF waeleza A-Z
- Get link
- X
- Other Apps
By
Maguruacademy
-
VIDEO: Serikali ya JPM yapongezwa kwa kupanua wigo wa ajira
- Get link
- X
- Other Apps
By
Maguruacademy
-
Messi na Ronaldo waburuzwa na samatta
- Get link
- X
- Other Apps
By
Maguruacademy
-
Messi, Samatta na Ronaldo. Mbwana samatta amechomoza katika orodha ya majina ya vinara wa mabao Cristiano Ronaldo na Lionel Messi ambapo mpaka wakati wa Krismasi na Mwaka mpya walikua wanaongoza lakini kwa mwaka huu imekua tofauti. Samatta ambaye ni nahodha wa Tanzania amejihakikishia kuwazidi Messi na Ronaldo kwa mabao ya ligi mpaka sasa baada ya jana kufunga bao 1 kwenye ushindi wa mabao 3-1 wa KRC Genk dhidi ya K.A.A. Gent jana. Kupitia bao hilo Samatta alifikisha mabao 15 hivyo kuwazidi Messi na Ronaldo ambao hawajafikisha idadi hiyo ya mabao. Ronaldo ana mabao 12 huku Messi akiwa na 14. Kwa mujibu wa ratiba ya ligi kuu ya Italia, Juventus imebakiza mechi moja kabla ya mwaka 2018 kumalizika ambapo itacheza dhidi ya Sampdoria Desemba 29 hivyo Ronaldo anahitajika kufunga mabao 3 ili kumfikia Samatta. Kwa upande wa Barcelona, wao hawatakuwa na mchezo mpaka mwakani hivyo Messi atabaki na mabao yake 14 ya ligi na kumwacha Samatta akiwa na mabao 15. Si...
Tundu Lissu kurudi Tanzania
- Get link
- X
- Other Apps
By
Maguruacademy
-
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu. Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amebainisha kuwa katikati ya mwaka 2019, anaweza kurudi nchini kwa ajili ya kuendelea na shughuli zake za kisiasa baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 Mwanasheria huyo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ametoa kauli hiyo akiwa anaendelea na matibabu nchini Ubelgiji. Lissu amesema "katikati ya mwakani naweza kurudi Tanzania, kuanza mazoezi hakutanizuia kurejea kwani naweza kurudi nyumbani na nikawa nakuja Ubelgiji kwa madaktari." Aidha kuhusiana na kugombea nafasi ya Urais kwenye Uchaguzi Mkuu 2020 Mwanasheria huyo wa CHADEMA amebainisha kuwa yuko tayari kukiwakilisha chama chake kwenye kinyang'anyiro hicho. "Wakikaa katika vikao na kunipa bendera ya kukiwakilisha chama changu, nitakubali kubeba msalaba huo mzito kwa mikono miwili" amesema Lissu.
Tabora:Wauguzi wanaotoa lugha chafu waonywa
- Get link
- X
- Other Apps
By
Maguruacademy
-
WAUGUZI na watoa huduma za afya wa zahanati, vituo vya afya na hospitali mkoani Tabora, wametakiwa kufuata maadili ya kazi yao na kuacha kutoa lugha chafu zenye maudhi au kebehi kwa akinamama wajawazito wanaoenda kupata huduma. Onyo hiyo, limetolewa juzi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Tabora, Mwajuma Mhina ambaye alisema baadhi ya akinamama wakiwemo wajawazito wamekuwa wakitendewa ukatili na wauguzi kwa kutolewa lugha chafu afya jambo ambalo ni kinyume na maadili ya kazi hiyo. Alisema wauguzi kama hao hawawezi kufumbiwa macho kwa kuwa vitendo vya vinadhalilisha utu wa mwanamke na kuwaomba kutoa huduma kwa kuzingatia maadili na misingi ya kazi. “Huu ni unyanyasaji kwa akinamama, unawezaje kutoa lugha zisizofaa wakati wa mgonjwa akihitaji umuhudumie, umesomea kuwahudumia huo ndiyo wajibu wako utimize.., lakini kwa kuwa wapo wasiosikia tunaiomba Serikali kupitia wizara ya afya kufuatilia na kuwachukuliwa hatua,”alisema. Al...
Z’bar: Naibu waziri atoa mazito kwa wanafunzi
- Get link
- X
- Other Apps
By
Maguruacademy
-
Na Khamis Sharif-ZANAIBAR NAIBU Waziri wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee ,Wanawake na Watoto, Shadya Mohamed Suleiman amewataka wanafunzi wa Jimbo la Magomeni kushughulikia masomo yao na kujiepusha na mambo ya tamaa kwani yanaweza kuwapelekea kutofikia malengo yao. Hayo aliyasema hivi karibuni alipokuwa akizungumza katika utaoji wa zawadi katika shule za Jimbo la Magomeni wakati wa sherehe ya utoaji wa zawadi kwa wanafunzi waliofaulu kuingia michepuo , kidato cha pili na kidato cha tano kwa mwaka 2017/2018. Alisema ili wafanikiwe zaidi katika elimu ni lazima wawe wasikivu na wavumilivu kwa kufuata ushauri wa walimu ndipo watafanikiwa kwani elimu ndio mustakabali mzima wa maisha na kuwataka waongeze bidii katika masomo kwani wao ndio wataalamu watarajiwa wa hapo baadae. “Acheni tamaa za kutamani vitu ambavyo wazazi hawana uwezo navyo mambo haya ndio yanayoweza kukuharibieni malengo yenu mliojiwekea ya b...
CCM Morogoro watoa sifa hizi
- Get link
- X
- Other Apps
By
Maguruacademy
-
i Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Morogoro kimewataka wananchi wote kumpa moyo Rais Dk. John Magufuli, kwani kazi anayoifanya chini ya serikali yake ni ya kishujaa kwa Watanzania wote. Pamoja na hali hiyo chama hicho kimewataka wananchi kuzidisha bidii ya kazi na uzalishaji wenye tija kwa manufaa pindi wanapokuwa kwenye ofisi zao, viwandani au mashambani. Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Innocent Kalogeresi alisema wananchi, viongozi , wanaharakati na wanasiasa , wote wana wajibu wa kutokuwa wepesi kurubuniwa au kununuliwa utu wao kwa kushiriki usaliti. “Rais Magufuli ni shujaa wa kweli wa maendeleo katika Taifa letu na kwa hali hii Watanzania wote kwa umoja na mshikamano wetu tumpe ushirikiano wa kila aina. “Tanzania ni moja na itabaki moja daima kwani ni miongoni mwa nchi yenye hazina kubwa katika nchi za Kusini mwa Afrika iliohifadhi wapigania...
Kampuni ya Setewico yalia
- Get link
- X
- Other Apps
By
Maguruacademy
-
Na MWANDISHI WETU-DODOMA UTITIRI wa kodi ambazo zinalipwa na wawekezaji nchini bado umeonekana kuwa changamoto kubwa kwao na hivyo kutoa ombi kwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk. John Magufuli kuangalia namna ya kupunguza utitiri huo wa kodi hizo. Ombi hilo limetolewa hivi karibuni jijini hapa na Mkurugenzi wa Ushirikiano na Uhusiano wa Jamii wa Kampuni ya Cetewico Limited, Katrin Boehl alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliofanya ziara katika kiwanda hicho. “Kwa upande wangu lazima niseme nimeona ushirikiano wa hali ya juu katika Serikali yangu Dodoma kwani nikiwa na tatizo lolote ninakwenda katika ofisi za Serikali yangu ya Dodoma, hivyo imeonesha uthamini wa kiwango kikubwa wa kazi tunazofanya,” alisema Katrin. Alisema kampuni yao inapongeza juhudi za Serikali katika ujenzi wa Tanzania ya viwanda nchini ili kufikia uchumi wa kati na wamedhamiria kuunga mkono kwa vitendo kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu lakini c...