Messi na Ronaldo waburuzwa na samatta
Messi, Samatta na Ronaldo.
Samatta ambaye ni nahodha wa Tanzania amejihakikishia kuwazidi Messi na Ronaldo kwa mabao ya ligi mpaka sasa baada ya jana kufunga bao 1 kwenye ushindi wa mabao 3-1 wa KRC Genk dhidi ya K.A.A. Gent jana.
Kupitia bao hilo Samatta alifikisha mabao 15 hivyo kuwazidi Messi na Ronaldo ambao hawajafikisha idadi hiyo ya mabao. Ronaldo ana mabao 12 huku Messi akiwa na 14.
Kwa mujibu wa ratiba ya ligi kuu ya Italia, Juventus imebakiza mechi moja kabla ya mwaka 2018 kumalizika ambapo itacheza dhidi ya Sampdoria Desemba 29 hivyo Ronaldo anahitajika kufunga mabao 3 ili kumfikia Samatta.
Kwa upande wa Barcelona, wao hawatakuwa na mchezo mpaka mwakani hivyo Messi atabaki na mabao yake 14 ya ligi na kumwacha Samatta akiwa na mabao 15.
Siku za hivi karibuni kumekuwepo na tetesi kwamba Mbwana Samatta anahitajika na klabu ya Ligi daraja la kwanza nchini England ya Middlesbrough.
Comments