UVCCM wampitisha mgombea Urais CCM 2020

Alhamisi , 27th Dec , 2018
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, kupitia kwa Katibu wa idara ya uhamasishaji na chipukizi Hassan Bomboko, imesema kuelekea uchaguzi wa mwaka 2020 umoja huo utaenda Dodoma kuhakikisha Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wa sasa Rais John Pombe Magufuli, anapewa
Umoja wa Viajana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM wakiwa kwenye kikao.
nafasi ya kuwania tena Urais.
Kwa mujibu wa Bomboko kwenye kikao kitakachofanyka Dodoma Umoja huo hautakuwa na lengo jingine zaidi ya kumpitisha Rais Magufuli kuwania tena nafasi hiyo ya kukiongoza chama hicho kwenye uchaguzi wa awamu ya pili.
"Kama msemaji rasmi wa UVCCM, msimamo wa taasisi yetu ni kwamba hatuna na hatutakuwa na mchakato wa kumtafuta mgombea Urais 2020 mwingine zaidi ya Magufuli ambaye ndiyo Mwenyekiti wa CCM" amesema Hassan Bomboko, UVCCM.
Aidha Bomboko amesema kuwa "mwaka 2020 tutakwenda Dodoma kwenye mchakato wa kidemokrasia Kukamilisha desturi yetu ya CCM ya kumbariki mgombea wetu kwa muhula wa pili, uchaguzi wa mgombea wa CCM tulishamaliza mwaka 2015"
"Kwa wenye nia ya kugombea Urais 2020 kupitia CCM watafute biashara nyingine ya kufanya kwani CCM hakuna Urais wa kupeana kiushemeji" ameongeza Hassan Bomboko.

Comments

Popular posts from this blog

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC