Huyu mama aamua kusema!



Mchungaji wa Kanisa la Assemblies Of God maarufu kama ‘Mlima wa moto’ Dk Getrude Rwakatare, amemshukuru Rais Magufuli kwa kumgundua Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam.

Mama Rwakatare amesema kuwa kwa mara ya kwanza alimuona Makonda ana bidii ya tofauti na jasiri.

"Namshukuru Rais wetu kwa kumgundua Paul Makonda , mimi nakumbuka nilikumgundua akiwa kiongozi wa Wana vyuo pale Moshi alivyonialika kwenye mkutano mkubwa kabisa wa wana vyuo," alisema Mama Rwakatare.

"Nilimuona ana bidii ya tofauti na ujasiri wa tofauti, niliona kwamba Mungu amempa wito ndani yake, nilikuiwa nasema Mungu naomba utokee mahali fulani kiwa bahati tukakutana tena kwenye Bunge la Katiba."

Mama Rwakatare ameyasema hayo katika hafla ya viongozi wa dini iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda ya kupata chakula cha pamoja.

Comments

Popular posts from this blog

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja