Tundu Lissu kurudi Tanzania

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amebainisha kuwa katikati ya mwaka 2019, anaweza kurudi nchini kwa ajili ya kuendelea na shughuli zake za kisiasa baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017

Mwanasheria huyo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ametoa kauli hiyo akiwa anaendelea na matibabu nchini Ubelgiji.

Lissu amesema "katikati ya mwakani naweza kurudi Tanzania, kuanza mazoezi hakutanizuia kurejea kwani naweza kurudi nyumbani na nikawa nakuja Ubelgiji kwa madaktari."

Aidha kuhusiana na kugombea nafasi ya Urais kwenye Uchaguzi Mkuu 2020 Mwanasheria huyo wa CHADEMA amebainisha kuwa yuko tayari kukiwakilisha chama chake kwenye kinyang'anyiro hicho.

"Wakikaa katika vikao na kunipa bendera ya kukiwakilisha chama changu, nitakubali kubeba msalaba huo mzito kwa mikono miwili" amesema Lissu.

Comments

Popular posts from this blog

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja