Mfungwa Apewa Adhabu Ya Kuangalia Filamu Jela
Jangili mmoja nchini Marekani ameamriwa kuangalia filamu ya wanyama ya Bambi kila mwezi baada ya kukutwa na hatia ya kuua “mamia” ya mbawala. Muwindaji huyo kutoka Missouri David Berry Jr anatakiwa kuangalia filamu hiyo walau mara moja kwa mwezi wakati akitumikia kifungo chake cha mwaka mmoja gerezani. Alitiwa nguvuni mwezi Agosti pamoja na ndugu zake wawili kwa kuwaua mbawala, kisha kuwachinja na kuondoka na vichwa huku akiacha miili ya wanyama hao ioze, waendesha mashtaka wamesema. Kesi hiyo ni moja ya kesi kubwa zaidi za ujangili kuwahi kuripotiwa kwenye historia ya jimbo la Missouri. Pamoja adhabu ya kwenda jela kwa kuwinda mbawala kinyume cha sheria, Jaji Robert George alimuamuru Berry Jr “kuangalia filamu iliyoandaliwa na kampuni ya Walt Disney iitwayo Bambi, ambapo alitakiwa kuangalia kwa mara ya kwanza kabla ama Disemba 23 na baada ya hapo kuangalia walau mara moja kila mwezi,” katika kipindi chote atachokaa jela. Filamu hiyo ya katuni ya mwa...