Yaliyo mkuta naibu Katibu Mkuu Chadema
RAYMOND MINJA-IRINGA NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) upande wa Zanzibar, Salumu Mwalimu, amekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa. Mbali na Mwalimu, wengine waliokamatwa ni Katibu wa Chadema wa mkoa huo, Jakson Mnyawami na Mwenyekiti wa Bavicha Wilaya ya Mbeya, Jailos Mwaijande. Viongozi hao walikamatwa jana wakijiandaa kuingia kwenye kikao cha ndani wilayani Mufindi kwa lengo la kujadili uchaguzi wa ndani wa chama hicho. Ilidaiwa kuwa hatua ya kukamatwa kwa viongozi hao ilitokana na agizo la Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamuhuri William kwa kuwa ofisi yake haikuwa na taarifa ya kufanyika kwa kikao hicho. Akizungumza na MTANZANIA, mbunge wa Viti Maalumu Chadema, Suzan Mgonakulima, alisema wameshangazwa na kitendo cha Mkuu wa Wilaya ya Mufindi kutumia Jeshi la Polisi kuzuia mkutano wao wa ndani ambao uko kisheria. Alisema walipofika kwenye ukumbi ambao walita...