RAIS JPM awajia juu wanasiasa wanaowatetea wafanyabiashara wasiolipa kodi
Rais John Magufuli, amewajia juu wanasiasa wanaowatetea wafanyabishara wasiolipa kodi na kuwataka kuacha mara moja huku akihimiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuwakamata wafanyabiashara hao haraka iwezekanavyo.
Ameyasema hayo leo Jumatatu Desemba 10, katika kikao maalumu kati yake uongozi wa TRA, na wakuu wa mikoa jijini Dar es Salaam ambapo amesema ni jukumu la kila Mtazania kulipa kodi.
“Kuna taarifa ya baadhi ya wafanyabashara kutetewa na wanasiasa, kwa hiyo Meneja wa TRA anamuachia, ukweli huo upo mimi ndiyo Mwenyekiti wa chama ninakwambia mshike.
“Baadhi yawafanyabiashara wameendelea kukwepa kodi kwa ujanja wa kuendeleza shughuli zauendeshaji, TRA kama kampuni kila siku inapata hasara kwanini isifungwe? Sisi hatuhitaji wawekezaji wanaopata hasara kila mwaka maana yake hiyo shughuli imemshinda,” amesema.
Aidha, amesema kuwa suala la kukusanya kodiha lina chama na kwamba ifike mahali watu wote walipe kwani wasipokusanya kodi nchi haitafika mahali.
Comments