TACRI yatoa neema Butiama

Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TaCRI) imefufua zao la kahawa wilayani Butiama mkoani Mara kwa kuanzisha vikundi vya wakulima baada ya zao hilo kutelekezwa kwa zaidi ya miaka 20 kutokana na ukosefu wa soko.

Hayo yameelezwa na Meneja wa Kanda wa Kituo cha TaCRI kilichopo Sirari wilayani Tarime, Almas Hamad akikabidhi  vifaa mbalimbali kwa ajili ya kilimo pamoja na mbegu kilo 5 za kahawa aina ya Chotala ili kuziotesha zitakazozalisha miche 25,000 kwa kikundi cha shamba darasa(SHADABI) kijiji cha Biatika kata ya Buhemba wilayani humo, alisema kuwa lengo ni kuwawezesha wakulima kujipatia kipato kitokanacho na kahawa.

‘’Tumeamua kufufua zao hili  wilaya ya Butiama,Serengeti na Rorya lililokuwa likilimwa miaka ya nyuma lakini likaachwa kutokana na sababu za ukosefu wa elimu ya kilimo bora na masoko, tutaanza na vikundi 5 hapa Butiama,Serengeti kipo kimoja na Rorya kimoja na kadri tunavyokwenda vikundi vitaongezeka’’alisema Hamad.



Aliongeza’’Tarime zao hilo limepiga hatua kubwa kwani kuna vikundi 17 na malengo yetu ni kuwa kwa Butiama vikundi vizalishe miche bora na mkakati ni kuhakikisha kwa mwaka inazalishwa miche 75,000 na tuwe na wakulima 1,500 ambao watakuwa mabalozi wa kufundisha wakulima wengine 5,000 na tunategemea ekali 250 ziwe zimepandwa na kila ekali miche 540 na kila mche utoe kilo moja ya kahawa safi.

Hamad alisema kuwa ukosefu wa soko la Kahawa ni changamoto kubwa inayorudisha nyuma kilimo cha Kahawa nakwamba TaCRI itakutana na bodi ya Kahawa na Ushirika ili kujadili namna ya upatikanaji wa masoko ambao ulisababisha wakulima wa Butiama,Serengeti na Rorya kutelekeza zao hilo

Afisa Kilimo na Umwagiliaji wilaya ya Butiama Reocatus Lutunda alisema kuwa wakulima walikuwa na hamasa ya kulima zao hilo lakini tatizo la bei liliwafanya wakulima kuacha kulima baada ya kutopata faida licha ya kutumia gharama katika kilimo hicho.

''Zao hili lilikuwepo na lilianzishwa kwa majaribio na lilionekana kufanya vizuri katika kata 7 ambazo vikundi viliundwa na waliuza kupitia ushirika lakini ikaonekana bei ni kidogo ikiuzwa sh. 40 ilipofika miaka ya 1990 badhi ya watu wakasusa wakaacha kulima,tuna mazao ya biashara zao la Pamba,na Alizeti na sasa Tumeongeza Kahawa''alisema Lutunda.

Comments

Popular posts from this blog

KESI YA ZITTO MUSWADA WA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA YAHAMISHWA

Waziri asimamisha likizo za Marubani ATCL