Wanawake viwandani Tanga wampa tano JPM utekelezaji sera ya viwanda


Wanawake wanaofanya kazi viwandani mkoani Tanga, wamemshukuru Rais John Magufuli, kwa utekelezaji wa vitendo wa sera ya viwanda na kwamba uwepo wa viwanda ni mkombozi kwa mwanamke.
Wakizungumza na Mtanzania Digital katika mahojiano maalumu katika Kiwanda cha Chokaa cha Neelkhanth Kilichopo JijiniTanga, baadhi ya wanawake kiwandani hapo wamesema utekelezaji wa sera ya viwanda unaofanywa na Rais magufuli ni mkombozi kwa mwanamke.
“Kazi nyingi za viwandani zimekuwa zikifanywa na wanawake jambo linalowakwamua na umasikini kwani kupitia hiyo nimeweza kutunza familia,” amesema Mwanamvua Ramadhani, mfanyakazi katika kiwanda hicho.
Amesema wanawake ambao hawana ujuzi pia wamepata fursa ya kupata ajira za muda mfupi katika viwanda mbalimbali nchini.
“Kama unavyofahamu wanawake tuna majukumu mengi hivyo kwa kweli utekelezaji kwa vitendo sera hii ni mkombozi, mwanamke kwa sasa kukaa nyumbani na kulia njaa ni kujitakia tu,” amesema Mwanamvua.
Kiwanda hicho ambacho kinacho tengeza chokaa kina wafanyakazi zaidi ya 3,000 na kati ya hao nusu ni wanawake na kwa mujibu wao wanashiriki kazi zote bila kuchagua.

Comments

Popular posts from this blog

KESI YA ZITTO MUSWADA WA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA YAHAMISHWA

Waziri asimamisha likizo za Marubani ATCL